Watu waache ujinga. Kuna posta pia zimo humu jukwaani zingine zinamtukana sakata, zingine huyo sijui Grealish.
Nimejaribu kupambana na watu humu lakini nimegundua asilimia kubwa ni viazi kabisa.
Mtu hata mpira wa makaratasi lakini domo refu kama la Mwajuma Kandambili.
Waliomtukana Grealish mpaka mama yake unashindwa kuelewa hivi huyu mtu ana maisha kweli? Wengine wanasema samata hajitumi, unajua kocha alimpa task gani uwanjani, au inadhaniwa ni kuufukuza mpira kila unapoenda? Wakina Ronado wamecheza mechi ngapi Italia kabla ya kuingia kwenye chemistry ya timu?
Acheni ujinga, umaskini wa akili huo. Mtanzania, Ya kwako yanakushinda unataka kuongoza cha mwingine tena kwa lugha ya dharau na kejeli.
Inaleta sana.!
Sent using
Jamii Forums mobile app