Watanzania tumelogwa, mchawi ni nani CCM au Upinzani??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
Rais kauliza swali leo na kujipa majibu!! Kasema tumelogwa , Swali kubwa lilikua ni kujiuliza nani katuroga. Kwa jinsi alivyokua akiongea kwa uchungu unaweza kutokwa na machozi!! Lakn swali linabaki pale pale!! NANI KATULOGA?? Nani mchawi wetu watanzania??

Tangu tupate uhuru tumetawaliwa na ccm , na ilani iliyotuongoza ni ya ccm, je kwa hali hii tutakua na mchawi mwingine zaid ya ccm???

Katiba ya nchi ndio mwongozo, kama rais aliye madarakan hatak tubadiri katiba bila shaka naye ni mchawi wetu watanzania, hawa wote tunaosema wakahojiwe kama ndio wachawi wetu , kuanzia mwanasheria mkuu mpaka mawaziri wa madini na makamishina. Wote hawa huwajibika kwa rais . Bila kuwagusa marais wastaafu tusitegee kuwajibishana.
Watasema nilifanya haya kwa maagizo toka juu!!

Rais JPM akitaka ajisafishe anze yeye kubadiri katiba kipengere kinacho mpa kinga ya kutoshitakiwa akiwa madarakan na akiacha madaraka . bila hivyo ni bure tu. Kingine anaita mikataba ya wenzie ipitiwe upya mbona mikataba yake ya kununua ndege hatak hata ijadiliwe bungeni?? Naye aweke mikataba alioingia hadhrani. Kuanzia reli mpaka ndege!! Vinginevyo tutampa ujiko rais ajaye atakapo itisha mikakata hiyo ipitiwe upya. Naye atamponda JPM na kujifanya yeye ni mzarendo. Na laan manunuzi yeyote yanayofanywa kwa siri na ikulu kwa kisingizio cha rais ni mzarendo!!

Wachawi wa nchi hii ni wana ccm!! Tunaomba mikataba ya sasa ya JPM mnakataa!! Akija rais mpya akisema tuipitie mikataba ya JPM mtashangilia!! Tuliomba gesi tusipitishe kwa dharula mkakataaa!! JPM anasema tupitie upya mnashangilia!! Tuliwaomba tupitie upya mikataba ya madini mlikataa JPM anasema tupitie upya mnashangilia!!

Wachawi wakubwa ni CCM NAWALAAAN SANA!!
 

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,312
2,000
Hakuna wa kulaumiwa, sheria na sera zetu mbovu zimeruhusu yote hayo kutokea.

Turudi square one tuanze upya.
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,769
2,000
hahaha kuna watu watajibu
TUNDU LISSU
[HASHTAG]#HappyAnniversaryToMeInJF[/HASHTAG]
 

tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
10,679
2,000
Jichawi ni chama chakavu yani baba mwizi,mtoto mwizi,babu mwizi,mama mwizi,bibi mwizi,mjukuu mwizi,kitukuu mwizi bila shaka umenielewaaaaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom