Watanzania tumelaaniwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tumelaaniwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JACADUOGO2., Aug 4, 2011.

 1. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa hayo matukio ya kifisadi yanayotokea hapa nchini na wananchi pamoja na viongozi tuko kimya tu nasema watanzania tumelaaniwa na hatuna akili timamu!

  1. Mtu mmoja anaiba trilioni 3 watanzania tuko tu kimya! TAKUKURU KIMYA, WABUNGE KIMYA NA SISI WANANCHI KIMYA? Nasema watanzania tumelaaniwa na hatuna akili timamu!

  2. Mtu anakodisha kiwanja cha ndege KIA na kila kitu ndani ya kiwanja kwa US $1,000 kwa mwaka? Watanzania tumelaaniwa na hatuna akili timamu!

  3. Tumeshindwa kukarabati reli ya kati leo tunataka tujenge reli mpya kutoka Tanga hadi Musoma! Hivi ni akili au matope?

  4. Shirika la ndege halina hata ndege halafu lina wafanyakazi 182! Aibu kwa taifa! Hivi hawa wafanyakazi wanafanya kazi gani? Watanzania hatuna akili timamu!

  5. Tuna bahari na maziwa ya kutosha lakini serikali haina meli! Ni bora Mungu angetunyang'anya bahari na hayo maziwa! Hatuna akili timamu!

  6. Mwekezaji kwenye mgodi anachukua 97% anatuachia 3%! Watanzania tuko kimya tu! Ni nani atakayetuondolea hii aibu?

  7. EPA, RICHMOND, DOWANS, UDA, IPTL, KAGODA nk aibu tupu!

  Hivi Tanzania ni nchi kweli au ni nchi ya kusadikika? Wananchi wa Tanzania tunategemea kwamba nani atatukomboa ktk upuuzi huu tunaofanyiwa na watu wachache kama siyo mimi na wewe?

  Leo hii watanzania tunalilia umeme wakati wengine wamejichimbia trilioni 3! Jamani!
  Leo hii bajeti ya uchukuzi inakwama wakati kuna watu binafsi wamejibebea pesa za watanzania mara tano zaidi ya pesa zinazotakiwa kukamilisha bajeti ya uchukuzi!

  Leo hii kuna baadhi ya wanafunzi wa UDOM wamezuiliwa kufanya mitihani yao kwa sababu ya madeni wakati wengine wamekumbatia pesa za watanzania!

  Kwa kweli nina mambo mengi sana ya kuandika lakini naomba niishie hapo kwani nina uchungu sana .
  MABADILIKO NDANI YA TANZANIA NI MIMI NA WEWE! MTANZANIA AMKA RASILIMALI ZETU ZINAISHA NA KUTOKOMEA!!
   
Loading...