Watanzania tujiandae ukosefu wa mafuta ghuba

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,681
WanaJF, niingie moja kwa moja kwny habari, kwamba watanzania tunatakiwa wote kujiandaa kisaikologia na ufahamu kuwa huenda tukapata uhaba mkubwa wa Mafuta ya magari kutokana na vita tarajiwa kati ya US na Iran.

Rais wa Marekani Jana aliamru mashambulizi dhidi ya Iran kuanzia Leo Ijumaa alfajiri kwa kulenga maeneo matatu muhimu ya kuanzia ambayo ni Maghala na viwanda vya silaha, vituo vya kurushia makombora na radar zote pia viwanja vya ndege vyote isipokuwa kiwanja kimoja tu hakijatajwa.

Imeelezwa kuwa tayari ndege 30 za mwanzo zilikuwa angani kusubiri amri ya mwisho kutoka kwa Rais.

Baadaye Leo dakika chache kabla muda kufika wa kuanza mashambulizi Bwana D. Tramph alisitisha kuanza kwa operation hiyo.

Chanzo: DW NEWS
Natumaini Mungu kasikia kilio cha wengi maana vita hiyo itaangamiza maelfu ya Raia wa Iran.

Je, wewe msomaji na mwanajf umejiandaje?
 
Mafuta yamepanda bei hadi kufika dola 64% kwa pipa (Oil Crude) hasa baada ya shambulio la UAV ya Marekani. Kama vita ikitokea ule ukanda basi tujiandae na mfumuko wa bei ambao haujawahi tokea,Tanzania yetu itakumbwa na hali mbaya sana maana kama bidhaa zitapanda bei kwenye hichi kipindi basi itakuwa balaa.

Pale the The Strait of Hormuz kwa siku yanapita mapima kama milioni 15 hadi 19 ya mafuta, hiki ni kiwango kikubwa sana cha utegemezi kuweza kufanya uchumi wa dunia uvurugike ndani ya muda mfupi tu.

Upande mwingine kuna hasara kubwa sana ambayo itatokea kwenye soko la hisa hasahasa pindi vita itakapoanza na watu kuanza kutoa pesa zao kuogopa hasara. Marekani kacheza kama pele kusitisha huu uvamizi maana hawezi kupigana vita ya kibiashara na wakati huohuo aingine kwenye mgogoro wa kijeshi na Iran

.
IMG_20190621_094708_637.jpeg
 
Afrika mafuta yapo lakini sijui tatizo letu nini kwa kweli! yaani kama wao wanapigana uko kwa upumbav.u wao, waafrika ilikuwa tuungane tuuziane mafuta wenyewe kwa wenyewe kwa bei nafuu.

Kupigana wapigane wengine, matatizo yaikumbe dunia nzima.
 
Back
Top Bottom