Watanzania tuifanye siasa kama msingi mkuu wa maisha yetu na si kama ushabiki

stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
430
Tutafeli kupiga hatua za maendeleo kama nchi sababu ya kufanya maamuzi magumu yenye maslahi ya taifa kishabiki, kama ushabiki wa simba na yanga.

Kuwa shabiki wa timu hizi huwa hakuambatani na sababu yoyote ya kimantiki,wala hoja yoyote ya msingi zaidi ya mtu kukwambia imetokea tu.

Sasa ktk siasa hupaswi kushabikia kitu bila kuwa na hoja wala mantiki,lakini haya ndiyo yanayoendelea nchini Tanzania.

Kwamba mtu hushabikia chama fulani huku hajui hata itikadi au sera za chama husika.Ukimuuliza anakwambia imetokea tu.Pia mtu hushabikia maamuzi fulani ya serikali au bunge bila kujua faida wala mantiki ya maamuzi hayo.Ukimuuliza anakwambia ni sababu chama changu kimetaka hivyo au imetokea tu

Ushabiki huu ndio uliotokea bungeni jana na pia hutokea mara kwa mara kwa wananchi pale raisi anapotumbua viongozi mbalimbali huku wananchi wakishabikia na kufurahia bila kutafiti ukweli au faida ya tukio husika.

Tatizo hili pia lipo ndani ya vyama vyote.Ambapo wanachama hushabikia maamuzi mbalimbali ya chama husika bila kuwa na hoja wala mantiki ya kushabikia.Pia ushabiki huu wa vyama huathiri maamuzi muhimu bungeni

Mambo ya ushabiki kwenye siasa husababisha kutokuhoji juu ya maamuzi mbalimbali,hivyo mambo yasiyo na maslahi kwa taifa kupita bungeni na pia maamuzi mabovu ya serikali kufanyika.Mwisho nchi yetu kuendelea kuwa maskini kama ilivyo kwa klabu zetu za simba na yanga.

Kwamba klabu hizi ni maskini wa uchumi na vikombe kimataifa kwa sababu ya mashabiki wao kutokuwekeza katika misingi ya soka badala yake kuwekeza ktk maneno matupu yasiyo na hoja wala mantiki yoyote kisoka.Ushabiki wa simba na yanga pia ndio ulioimaliza fimu ya taifa.

Ushauri tusishabikie siasa kama ushabiki wa simba na yanga .Siasa ni maisha,kwa maana maamuzi ya kisiasa yanaathiri maisha yetu sote kama watanzania kiuchumi na kijamii.Hivyo tuichukulie siasa kama suala nyeti linalohitaji utafiti na hoja zenye mantiki kabla ya kushabikia
 
Back
Top Bottom