Nkuba25
JF-Expert Member
- Nov 18, 2015
- 2,341
- 13,021
Katika ufuatiliaji wangu wa mada mbalimbali humu, nimekuja kugundua Watanzania ni watu wa kuendeshwa na matukio na wamejawa na mihemko.
Hili jambo kama Taifa linatufanya tushindwe kupiga hatua na kubaki kuwa watu wa porojo tu pasipo vitendo.
Sasa hivi Taifa zima limegeukia swala la Lugumi na Jeshi la Polisi. Hii ndio habari ambayo yatu wapo busy kuijadili kwa mihemko ya hali ya juu.
Yaani sasa hivi tumeshasahau maswala kama:
1. RAIA wa China kujazana kariakoo na kufanya biashara ambazo zilitakiwa kufanywa na watanzania.
2. Raia wa kigeni kujaa Tanzania na kufanya Kazi bila vibali. Wachina ndio wanaongoza, na kama mtakumbuka ile kamata kamata ilipoanza, Balozi wa China alifanya "Chinese Night Party" na mgeni rasmi alikuwa waziri Charles Kitwanga, na baada ya hapo hilo zoezi likakoma.
3. Ishu ya January Makamba kuwaibia pesa "wawekezaji" kwa ahadi za kuwapatia Kazi.
4. Ishu ya waziri Muhongo kumpenyezea taarifa ya siri Mkuu wa wakala wa vipimo juu ya ujio wa waziri Mkuu kwa hiyo afungulie zile mita. Tulitarajia waziri Muhongo nae awajibishwe kwa sababu (a) alikuwa anajua zile mita hazifanyi Kazi lakini hakuchukua hatua yoyote (b) kutoa taarifa za siri za utendaji wa waziri Mkuu. Lakini hadi Leo Muhongo anapeta.
5. Kesi ya Kamishana Mkuu Wa TRA Rashed Bade, huyu kamishna Mkuu alisimamishwa Kazi kutokana na ubadhirifu uliokuwa unaendelea pale TRA. Sasa mmeshawahi kujiuliza mbona hapelekwi mahakamani?
6. Ufisadi wa NIDA. Tulishuhudia yule mkurugenzi wa NIDA Jackson Mwaimu akisimamishwa kazi pamoja na wakuu wenzake pale NIDA, sasa mmeshawahi jiuliza hili swala limeishia wapi? Mbona hatuoni wakipelekwa mahakamani?
7. Na mengineyo mengi.
Hayo maswala tajwa hapo juu, nayo yalijadiliwa kwa mihemko ya hali ya juu sana. Wote tukiamini Rais JPM anaenda kutenda kitu katika hayo, lakini yamezimika ziiiii...
Sasa kama Taifa, tutashindwa kuiwajibisha serikali kwa vitendo, hakika daima tutaendelea kubwabwaja humu kwenye mitandao ya jamii mpaka mwisho wa maisha yako.