Watanzania, ni Ujinga kuikubali pipi kwa matarajio ya kuondoa njaa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa, mtu mwenye nia ovu akikudanganya na wewe ukaupokea uwongo wake anakudharau.

Rais Obama aliwahi kutamka kuwa Afrika haiendelei kwa sababu viongozi wake badala ya kutumia muda wao mwingi kufikiria namna ya kuwaletea watu wao maendeleo, wao wanatumia muda wao mwingi kufikiria namna ya kubakia madarakani.

Mwalimu Nyerere aliwahi kunena tena, akimnukuu mwanafalsafa mmoja kuwa, viongozi wazuri ni wanafalsafa, lakini wanafalsafa wengi hawauhangaikii oungozi. Kwa hiyo viongozi wengi ni wale wasio na sifa za kuwa viongozi.

Na kuna mwanafalsafa mwingine aliwahi kunena, adhabu ya watu wengi wenye akili kubwa kutogombea uongozi ni kutawaliwa na wasio na akili.

Na mimi nasema, kama una njaa, usikubali kupokea pipi kwa matarajio ya kushiba, zaidi itafubaza akili na jitihada zako za kutafuta chakula kwa utamu wa mdomoni, huku tumbo lako likibakiwa na njaa, na viungo vyako vikizidi kunyong'onyea.

Tatizo kubwa la Afrika, linalolifanya bara hili kuwa la giza, ni mifumo mibaya inayosimamia uchumi ambayo nayo inasababishwa na tatizo la uongozi. Ukizungumzia sheria mbaya za kodi, ni uwezo mdogo wa viongpzi. Ukizungumzia matatizo ya rushwa, unazungumzia tatizo la uadilifu mdogo wa viongozi. Ukizungumzia uduni wa elimu, tekinolojia, haki, demokrasia, vyote chanzo kikubwa ni viongozi. Biblia inasema, kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie, au la wote watatumbukia shimoni. Afrika inahitaji mifumo iliyo bora kabisa, ya kuwapata walio bora kabisa kuwaongoza waliosalia katika ngazi zote, toka chini mpaka juu. Tatizo kubwa, watawala wa Afrika wameziba kabisa uwezekano wa kupata mifumo kama hiyo ili tu kakikundi kadogo kaweze kutawala hata kama hawana uwezo wa kuja na mbinu mpya za kuleta mwanga Afrika.

BACK HOME

Kwa Tanzania, kizingiti kikubwa cha kujenga mifumo bora kabisa ya kiutawala na kiuongozi ni CCM, ambayo siku zote inafikiria namna ya kuendelea kubakia madarakani badala ya kufikiria namna ya kuiletea maendeleo Tanzania. Uchawa na unafiki unalenga kubakia madarakani, siyo kuleta maendeleo kwa nchi.

Ebu sikiliza viongozi wa Serikali au hata viongozi wa CCM, ni lini uliwahi kusikia CCM imeandaa kongamano la kujadiliana na wananchi namna ya keleta maendeleo mahali fulani? Kila mahali utawasikia viongozi wa CCM, mara ooh CCM itatawala milele (loh! una akili wewe? Hivi chama fulani kutawala milele au muda mfupi kuna mchango gani kwa nchi), mara ooh, wananchi hawali katiba, wanataka maji (una akili wewe? Hivi hata hayo maji yatapatikana kwa ubora bila kuwa na mifumo bora inayounda sera, inayojenga uchumi ili pesa na utaalam vipatikane?). Mara ooh, Samia ndiyo mgombea pekee 2025 (ni ujinga sahizi kuzungumzia nani awe mgombea na nani asiwe, badala ya kuzungumzia ujenzi wa taasisi imara za kusimamia demokrasia, mifumo itakayolihakikishia Taifa ustawi bila ya kuangalia nani anatuongoza).

Tuna matatizo makubwa ya msingi ambayo hayawezi kutatuliwa kwa kuyapaka mafuta badala ya kuyaondoa. Na utatuzi wake ni lazima uanzie kwenye msingi. Tukubali kuwa nyumba yetu ni dhaifu kwa sababu msingi wake ni dhaifu. Kama tunataka ustawi wa Tanzania, lazima tuanze na katiba, maana ni kwayo ndiyo mambo mengine yote yanajengeka. Mambo ya kusema, sijui Tume huru ya uchaguzi, sijui mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, ni kama una njaa, badala ya kutafuta chakula, na kuhakikisha una unakuwa na uwezo wa kuwa na chakula chako wakati wote, wewe unatafuta pipi ukitegemea kushiba! Matatizo ya nchi hii, siyo uchaguzi pekee yake bali ni mifumo karibia yote ya kiutawala, usimamizi, maamuzi, n.k. Haya hayatatuliwi na Tume Huru ya Uchaguzi.

Watanzania ni lazima waende kwenye msingi wa Tatizo, na anayetaka kutupatia pipi akituaminisha ndiyo suluhu ya njaa, ahesabike ni adui yetu kwa sababu anataka kuifubaza na kuihadaa akili yetu kwa utamu wa mdomoni wakati siyo ufumbuzi wa tatizo letu la Msingi.

Tanzania, tukiwa na msingi imara, tunaweza kuwa Edeni ya Duniani:

1) Sisi ni majasiri kweli wa ujinga. Tunawezaje kuwa na uhaba wa maji huku ndiyo nchi inayoongoza kwa uwingi wa fresh water bodies?

2) Sisi ni majasiri kweli wa ujinga. Tunawezaji kuwa na mgao wa umeme, huku tuna maji mengi, gas, makaa ya mawe, upepo na jua? Ni ujasiri wa kijinga wa hali ya juu kusimama juu ya kijinga cha moto huku kikiunguza mguu wako, huku kuna eneo kubwa lisilo na moto.

3) Sisi ni majasiri wa hali ya juu wa ujinga. Tunawezaje kuzungumzia upungufu wa chakula wakati tuna ardhi kubwa yenye rutuba, tuna maji mengi, tuna watu wengi wanaozunguka tu mitaani wakilalamikia kutokuwa na kazi.

4) Sisi ni majasiri wakubwa wa ujinga Duniani. Tunawezaje leo, wafanyabiashara zaidi ya 90% kuwa wachuuzi wa bidhaa duni kabisa za China wakati huko nyuma tulikuwa na bidhaa za aina hiyo hiyo, tena za viwango vya juu ambazo ubora wake, hizi bidhaa takataka za kutoka China haziwezi kuzifikia hata kwa 50%, lakini tukaziua ili tusiwe wazalishaji, tuwe wachuuzi wa bidhaa takataka za China.

Haya yote yanaendelea huku viongozi wakishangilia. Tena wengine wakijagamba kuwa sasa hivi nchi imepata maendeleo makubwa.

1) Utawezaje kusema tuna maendeleo makubwa wakati tulikuwa tunaunganisha magari na matrekta, leo hatuna hata kiwanda cha kuunganisha magari?

2) Utawezaje kusema tumeendelea sana wakati zamani tulikuwa na kiwanda cha kutengeneza baiskeli ya brand ya swala, sahizi hatutengenezi hata sindano?

3) Utawezaje kusema tumeendelea wakati zamani tulikuwa tunatengeneza viatu, nguo bora, matairi, majembe, leo vyote, tunaagiza toka China, tena vyote vikiwa na uduni wa hali ya juu?

4) Utawezaje kusema tumeendelea sana, wakati hapo zamani tulikuwa tunaongoza Duniani kwa uzalishaji wa katani, leo hakuna hata zao moja ambalo tunaongoza kwa uzalishaji?

5) Unawezaje kusema tuna maendeleo ya teknolojia wakati zamani tuliweza kutengeneza gari la brand ya nyumbu lakini leo hatutengenezi hata pikipiki?

Ukweli ni kwamba tunayafurahia maendeleo ya Dunia lakini siyo maendeleo ya Taifa letu. Sisi tumerudi nyuma wakati Dunia inaenda mbele kwa speed kubwa.

TUTAFAKARI

Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru, nchi yetu ilikuwa kwenye kiwango sawa na Singapore, Thailand, Indonesia na Malaysia. Taarifa ya UNDP ya miaka kama mitano iliyopita inasema kuwa Tanzania ikiendelea na speed yake ya maendeleo ya sasa hivi, na Malaysia wakabakia pale pale walipo leo, itatuchukua miaka zaidi ya 250 kuwafikia. Chanzo cha utofauti huu kati yetu na mataifa haya mengine ambayo awali tulikuwa sawa ni nini? Ni UONGOZI. Wenzetu waliwapata watu wenye maono, wenye dhamira safi, wanaofikiria maendeleo ya mataifa yao kuliko kutumia muda mwingi kupanga mbinu chafu za kubakia madarakani, wakawaongozi kupata mifumo imara ya kuwaongoza kuyafikia maendeleo.

WATANZANIA WA KAWAIDA NA VIONGOZI WENYE DHAMIRA NJEMA, TUUNGANE KATIKA KUJENGA MIFUMO IMARA YA KUTUONGOZA KUYAFIKIA MAENDELEO. KAMA CCM NDIYO KIZINGITI CHA KUFIKIA USTAWI WA NCHI, WANANCHI TUITANGAZE KUWA NI ADUI WA TAIFA NA WATANZANIA WOTE. TUANZE NA KATIBA.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa, mtu mwenye nia ovu akikudanganya na wewe ukaupokea uwongo wake anakudharau...
Fikiria vizuri Bams..CCM is just a political party, they are nothing! Aliyeko nyuma ya ccm ndiye tatizo..find out who is behind ccm, that's where the problem lies.
 
dah kwanini nimezaliwa Afrika 😭😭 sijui Afrika tumemkosea nini M/MUNGU,tuliowaamini hawana habari na wananchi wao
 
Huwa nakuelewa sana Mkuu BAMS..ila tusichoke,tuendelee kutoa ELIMU ya URAIA kwa UMMA,naamini soon tu waTz wataamka..

Labda niwaombe CHADEMA watumie hii fursa ya vijana wengi kuhitimu elimu ya Kidato cha Nne,hasa baada ya kujengwa kwa shule nyingi ngazi ya Kata..LICHA ya mapungufu ya ubora wa Elimu walioipata mashuleni,NAAMINi wao ni BORA kuliko walioishia darasa la Saba(7)
 
Viongozi hao wanatokana na Jamii tuliyopo so ukiona kila kiongozi ni wa hovyo hiyo ni maakisio ya kwamba na Jamii yenyewe pia ni ya........ Kazi Tunayo
 
Fikiria vizuri Bams..CCM is just a political party, they are nothing! Aliyeko nyuma ya ccm ndiye tatizo..find out who is behind ccm, that's where the problem lies.

CCM kama chama cha siasa, kingekuwa kweli ni chama cha siasa, wala kisingekuwa na mchango mkubwa kwenye mifumo yetu mibaya.

LAKINI kiuhalisia CCM siyo chama cha siasa, ni dola iliyojificha ndani ya Serikali. Ndiyo maana wakati wote wanataka Rais ndiye awe mwenyekiti wa chama ili aitumie dola kutekeleza matakwa ya chama.

Hivi hata leo hii akija Samia kwenye shughuli za chama, wewe mwanacha wa CCM una uwezo wa kusimama mbele yake, ukawa na nguvu, ya kumhoji kama Mwenyekiti wako wa CCM?
 
Viongozi hao wanatokana na Jamii tuliyopo so ukiona kila kiongozi ni wa hovyo hiyo ni maakisio ya kwamba na Jamii yenyewe pia ni ya........ Kazi Tunayo
Hilo ni kweli, unakuta mtu anaamini uongozi ni fursa kama fursa zengine tu za kimaisha halafu unakuta mtu huyo huyo naye anashangaa Tanzania kuwa na viongozi ambao wanajali sana madaraka kuliko kufikiria maendeleo ya nchi wakati kumbe hao viongozi wanatoka kwenye jamii yenye fikra kama zake.

Tanzania si viongozi tu wa nchi ndio tatizo bali hata ukiangalia sekta zengine utakuta kuna watu upeo na mitazamo yao ndio ile ile kama ya viongozi wa nchi na ndio maana hatuna kitu tunachokifanya kwa ubora chenye kututangaza duniani zaidi ya kutwa kujisifu na amani kama tumeambiwa dunia nzima ipo vitani na sisi tu ndio hatuna vita.
 
Viongozi hao wanatokana na Jamii tuliyopo so ukiona kila kiongozi ni wa hovyo hiyo ni maakisio ya kwamba na Jamii yenyewe pia ni ya........ Kazi Tunayo
Unachosema ni sahihi. Lakini kila jamii, japo wanaweza kuwa wachache, lazima kutakuwepo watu wenye ubora katika jambo lolote lile iwe katika uongozi, tekinilojia au fani yoyote ile.

Tatizo la nchi za Afrika, na hasa Tanzania, hakuna mifumo ya hao cream kupenya na kukalia yale maeneo ambayo wanayamudu kwa kiwango cha juu kabisa. Tatizo ni mifumo mibaya ya kiutawala

Ebu fikiria Rais anapokuwa ndiye mtu wa kuteua watu wote wa kuongoza/kusimamia maeneo yote ambayo ni determinants ya maendeleo ya nchi yetu. Huyu Rais ana akili ya kiasi gani, ana macho ya kiasi gani, ana uelewa wa taaluma zote kwa kiasi gani, hata awatambue watu wote walio wazuri kabisa katika fani zao? Watasema kuwa wanafanyiwa vetting na watu wa TISS, lakini huko TISS kwenyewe ni shida tupu. Wengine ni watu wa hovyo kabisa. Wamegeuza umbeya kuwa profession. Hao watamsaidia Rais kuwapata watu wazuri?
 
Inasikitisha Sana.

Hatuna viongozi bali tuna wachumia tumbo.
Wengi wanatafuta uongozi kama njia za kutegemeza maisha yao.

Kwa nchi kama hizi zetu, ilistahili kuwafanya viongozi kuwa na malipo ya chini lakini wahakikishiwe mahitaji ya lazima ili waende kwenye uongozi watu wenye dhamira ya kuona nchi yetu inatoka mahali ilipo. Lengo liwe kuwaondoa waroho wa fedha na wataka utajiri kupitia uongozi. Kwa sasa, umashangaa kabisa, watu crooks, alimradi ana vihela vya kuhonga, anataka uongozi. Sasa mtu aliyepata vihela kwa kupora ataweza kuweka mifumo ya kuwafanya watu wapate hela halali?
 
Huwa nakuelewa sana Mkuu BAMS..ila tusichoke,tuendelee kutoa ELIMU ya URAIA kwa UMMA,naamini soon tu waTz wataamka..

Labda niwaombe CHADEMA watumie hii fursa ya vijana wengi kuhitimu elimu ya Kidato cha Nne,hasa baada ya kujengwa kwa shule nyingi ngazi ya Kata..LICHA ya mapungufu ya ubora wa Elimu walioipata mashuleni,NAAMINi wao ni BORA kuliko walioishia darasa la Saba(7)
Ni kweli, kwa kiasi kikubwa Elimu ni mkombozi wa kila kitu. Na ndiyo maana hata kwenye ule utafiti wa TAWEZA ilionekana wazi kabisa kuwa CCM ilikuwa ikiungwa sana mkono na watu wenye yelewa duni/watu wajinga.

Wasomi wengi walionekana kuunga mkono zaidi vyama vya upinzani. Bila ya kujali wasomi hao walikuwa wanaunga mkono chama gani, kilicho dhahiri ni kwamba kutouiunga mkono CCM, ina maana wabatambua wazi kuwa kuna mambo yanayofanywa na CCM kupitoa Serikali yake, siyo sahihi.
 
CCM kama chama cha siasa, kingekuwa kweli ni chama cha siasa, wala kisingekuwa na mchango mkubwa kwenye mifumo yetu mibaya.

LAKINI kiuhalisia CCM siyo chama cha siasa, ni dola iliyojificha ndani ya Serikali. Ndiyo maana wakati wote wanataka Rais ndiye awe mwenyekiti wa chama ili aitumie dola kutekeleza matakwa ya chama.

Hivi hata leo hii akija Samia kwenye shughuli za chama, wewe mwanacha wa CCM una uwezo wa kusimama mbele yake, ukawa na nguvu, ya kumhoji kama Mwenyekiti wako wa CCM?
Bams dola siyo jini ni watu..je ni wangapi, wako wapi..nk
 
CCM is the political wing of TISS AND TPDF.
 
Bams dola siyo jini ni watu..je ni wangapi, wako wapi..nk
Dola siyo mtu mmoja bali kikundi cha watawala pamoja na taasisi zinazotumika kujenga maguvu ya Serikali. Watawala hawa ndio wanaoamrisha vyombo vya dola. Taifa likiwa linaongozwa na wenye hekima wanaopenda na kutenda haki, vyombo vya dola vitatumika kulinda haki. Watawala wakiwa ni watu wanaogandamiza haki, basi vyombo vya dola husimamia ugabdamuzaji wa dola.

Mathalani, watu wana haki ya kukusanyika iwe ni chini ya vyama vya siasa, vikundi vya kijamii au taasisi za dini, Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alipotoa amri ya kukanyaga haki na katiba, kuwa vyama vya upinzani haviruhusiwi kufanya mikutano, wanaosimamia huo ugandamizaji wa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano, ni Polisi na TISS, na viongozi wa Serikali kama maDC na maRC. Lakini tamko lile lilitolewa na Mwenyekiti wa CCM kwa maslahi ya CCM lakini kutumia ofisi ya Rais.
 
CCM is the political wing of TISS AND TPDF.

Kimsingi CCM haina sifa kabisa ya kuitwa chama cha siasa. Ni sydicate ya watu fulani walioteka nchi kwa kupitia ulaghai dhidi ya umma, na kisha kupokonya dola. Leo hii siyo wananchi wanaoamua nani awe Rais au mbunge, bali ni hiki kikundi kinachotumia jina la CCM kuendelea kushikilia dola waliyoipokonya toka kwa umma.

Fikiria mwaka 2020, wagombea wote wa ubunge kupitia CCM, 75% ni waliokataliwa na wajumbe. Kama wajumbe waliwakataa, ni nani aliyewateua?
 
Unachosema ni sahihi. Lakini kila jamii, japo wanaweza kuwa wachache, lazima kutakuwepo watu wenye ubora katika jambo lolote lile iwe katika uongozi, tekinilojia au fani yoyote ile.

Tatizo la nchi za Afrika, na hasa Tanzania, hakuna mifumo ya hao cream kupenya na kukalia yale maeneo ambayo wanayamudu kwa kiwango cha juu kabisa. Tatizo ni mifumo mibaya ya kiutawala

Ebu fikiria Rais anapokuwa ndiye mtu wa kuteua watu wote wa kuongoza/kusimamia maeneo yote ambayo ni determinants ya maendeleo ya nchi yetu. Huyu Rais ana akili ya kiasi gani, ana macho ya kiasi gani, ana uelewa wa taaluma zote kwa kiasi gani, hata awatambue watu wote walio wazuri kabisa katika fani zao? Watasema kuwa wanafanyiwa vetting na watu wa TISS, lakini huko TISS kwenyewe ni shida tupu. Wengine ni watu wa hovyo kabisa. Wamegeuza umbeya kuwa profession. Hao watamsaidia Rais kuwapata watu wazuri?
Inasikitisha sana. Chukua hii nyingine..... 'Kiongozi msafi katika mfumo mchafu hugeuka na kuwa sehemu ya mfumo '........ Kazi ipo hii nchi
 
Back
Top Bottom