Watanzania nani katuloga?

Watanzania nani katuloga?

SECONDLADY

Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
14
Reaction score
12
Kwa wale ambao ni Wakristo, mtakumbuka Mtume Paulo katika Wagalatia 3:1 aliwaambia Watu wa Galatia maneno haya, "Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?"

Naomba nitumie mtazamo huu, kuwauliza watanzania kuwa ni nani aliyetuloga? Miaka zaidi ya 50 tangu tupate uhuru bado tunadanganywa na wanasiasa uchwara na ahadi maelfu yasiyotekelezeka na bado tunashabikia na kupokea kanga na kofia tunakubali kudanganywa, ni nani aliyetuloga?

Ni nani aliyetuloga kuwa kujiuzulu kwa mawaziri wanne ili kumuokoa Pinda kutasaidia kurekebisha matatizo ya nchi hii? Ni nani aliyetuloga kuwa tutakuwa na maisha bora kwa kubadilisha watu wale wale, wenye fikra zile zile, miaka nenda miaka rudi?
 
Ni nani aleituloga sisi watanzania wajinga?ongeza neno wajinga ili ilete maana zaidi,labda tumelogwa na magamba.
 
Back
Top Bottom