Watanzania Mnatunza kumbukumbu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Mnatunza kumbukumbu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by jaxonwaziri, Aug 5, 2010.

 1. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 377
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Hivi majuzi tu huyu bwana alisema yaliyopo hapa chini, wengi sana tukaumizwa kwa ulevi huu na jeuri. Tukajiuliza anatoa wapi jeuri ya kejeli hii?
  View attachment 12285  Je, watanzania, tutakumbuka ufinyu wa fikra zake na kuamua kumfunza adabu yeye, na wenzake wote wanaopewa dhamana na wananchi na baadaye wanaanza kuwadharau wananchi hao hao waliompa dhamana husika?
  Tusifanye makosa, hatuhitaji viongozi wa namna hii, kwanza naombeni msamaha kwenu ninyi watu mlio makini humu jamvini kwa kumuita jamaa huyu "kiongozi". Neno kiongozi lina maana ya pekee na inayostahili kuheshimiwa. Ila huyu, ni picha tu, yupo pale kucheka cheka tu!
  Kura zote kwa Dr Wilbroad Slaa pamoja na wabunge wa upinzani, chagua CCM pale tu, mbunge wa CCM ni mtu makini na ameonyesha utendaji uliotukuka katika historia ya uongozi wake!
  Tumeona madudu wanayoyafanya katika chaguzi. Wanatabia ya zengwe na wizi uliokithiri. Pia rushwa na kila aina ya uozo! Tumeshuhudia kwa wazi kabisa utumikaji wa mbinu chafu ili kupata nafasi za uongozi, tujiulize tukiendelea kukabidhi taifa kwa watu kama hawa, tutekuwa tunaipeleka wapi Tanzania? Jibu ni rahisi, HATUWATAKI na katika karatasi za kura mwaka huu tutawaeleza wazi kuwa "WAMEOZA" na "TUMEWACHOKA"
   
 2. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkakati uliobaki ni kuwashawishi ndugu zetu wa mikoani kwa kuwa kuna watu bado wanavaa hiyo fulana.!!!!!!
   
 3. R

  Ramos JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yap. lakini mkakati muhimu zaidi kwa sasa ni kulinda kura. Ukweli ni kuwa CCM hawana namna nyingine ya kushinda mwaka huu zaidi ya kuiba...
   
 4. J

  Jafar JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji kampeni ya kisasa ili Dr. Slaa ashinde. Kampeni za majukwaani hazitoshi. Tuige kamati ya Obama, walitumia sms, e-mail, pens etc kumfikia kila mtu nyumbanin kwake. Tunahitaji mbinu ya kumfikia mtu nyumbani kwake aelewe bila ya kubughuziwa ili akitoka hapo nyumbani tarehe 31 Octoba aende kuchagua CHADEMA.

  Changua CHADEMA 2010
   
Loading...