Watanzania mbona hamjahoji uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa bei ya kutupwa?

Umekosea namna ya kuuliza hilo swali, watanzania tuliisha hoji uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa. Ila wanaCCM walipingana na watanzania juu ya uuzwaji wa nyumba hizo kwa bei ya kupeana.
 
Kwa sasa watanzania (walio wengi) wanasherehekea kutumbua majipu. Naomba niwakumbushe nyumba za serikali ziliuzwa bei ya kutupwa mbona hampigi kelele jipu hilo likatumbuliwa?
Ikipita miaka 25 itakuwa fait accompli. Sasa hivi itakuwa imekaribia miaka 15, Kama siyo zaidi
 
shshshshhh!! ongea polepole. si unajua hili linamhusu mtumbua majipu? na watu hawataki kusikia anakosolewa kabisaaa! kwani hata suala la ile ferry mbovu ya dar-bagamoyo unalisikia? unataka watu waandamane humu Jf na mabango ya kumtetea?
Jamani si kuna mahakama ya mafisadi imeshafika.
 
shshshshhh!! ongea polepole. si unajua hili linamhusu mtumbua majipu? na watu hawataki kusikia anakosolewa kabisaaa! kwani hata suala la ile ferry mbovu ya dar-bagamoyo unalisikia? unataka watu waandamane humu Jf na mabango ya kumtetea?
Mtu akishakuwa kiongozi wa nchi tunatakiwa tumheshimu na kumheshimu ni pamoja na kutokuanza kufungua mabaya yake hata kama tunayajua.Huyu ni kiongozi mkuu mapungufu yake madogo madogo yawekwe kando kwanza,tumkosoe kwa haya ya sasa.Umenielewa???
 
Kwani nai aliuza nyumba hizo?
 
Mtu akishakuwa kiongozi wa nchi tunatakiwa tumheshimu na kumheshimu ni pamoja na kutokuanza kufungua mabaya yake hata kama tunayajua.Huyu ni kiongozi mkuu mapungufu yake madogo madogo yawekwe kando kwanza,tumkosoe kwa haya ya sasa.Umenielewa???
Nimekuelewa, kwahiyo tuna encourage selective prosecution?
 
Mtanzania gani wa kushikia bango mambo kama haya?

"Watawala" wetu wanatujua vizuri. Wanajua udhaifu wetu. Wanajua tunavyoridhishwa na maamuzi ya "kimedia". Wanakiri makosa na kuahidi kuchukua hatua lakini ndio imetoka.

Wanajua kwa akili hizi hatutakumbuka. Wachache wenye akili angalau nao wana njaa mbaya. Wakiahidiwa kushiba wanageuka wapiga zumari wa viongozi. Aibu, aibu, aibu!!!
 
Mtanzania gani wa kushikia bango mambo kama haya?

"Watawala" wetu wanatujua vizuri. Wanajua udhaifu wetu. Wanajua tunavyoridhishwa na maamuzi ya "kimedia". Wanakiri makosa na kuahidi kuchukua hatua lakini ndio imetoka. Wanajua kwa akili hizi hatutakumbuka. Wachache wenye akili angalau nao wana njaa mbaya. Wakiahidiwa kushiba wanageuka wapiga zumari wa viongozi. Aibu, aibu, aibu!!!
Nimeridhika na uandishi wako, unawajua fika watanzania! Sina la kuongeza- wale wa musoma etc
 
Back
Top Bottom