Watanzania, Mbaya Wetu ni Katiba Yetu!!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Nasema bado tutaendelea kupigwa!

Ikiwa katiba tuliyonayo bado itaendelea kutoa hakikisho la kutoshtakiwa kwa marais wastaafu kwa makosa yote watakayoyafanya wakiwa madarakani.
Tunashangaa nini lipi kwa haya yanayotokea sasa?
Hivi unadha kama katiba yetu hii ingekuwa inaruhusu hawa marais wastaafu kushtakiwa kwa makosa waliyoyafanya hali ingekuwaje?
Unadhani kungekuwa na huu uhuni unaoendelea katika sekta ya madini na nyinginezo.
Hayo ya mikataba ya madini ni mambo ya Mkapa hapo bado hatujaja kwenye mikataba ya gesi na Kikwete.

Narudia kusema tena sisi bado mbaya wetu ni katiba mbovu waliyoikumbatia ccm maadamu inawabeba kwa sehemu fulani.
 
HATUHANGAIKI NA KATIBA, KAMA KATIBA NI MBAYA, MBONA VIONGOZI WA CHADEMA WALIAPA KUILINDA?
 
HATUHANGAIKI NA KATIBA, KAMA KATIBA NI MBAYA, MBONA VIONGOZI WA CHADEMA WALIAPA KUILINDA?
Ndio zako ila siku mheshimiwa akisema hii ni katiba mbaya bila shaka utaunga mkono tu kama ulivyokuwa ukiunga mkono wakati wa kusaini mikataba ya madini,
 
Magufuli mwenyewe anajichetua tu. Hana nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania. Kama ana lengo zuri kweli, basi abadilishe mifumo iliyojengwa na katiba yetu mbovu. Kwahiyo abadilishe katiba, siyo kubadilisha watu.
 
Kweli kabisa,bila katiba imara itakayobadilisha mfumo wa utawala tutarajie ufisadi Kwa sana.Mkataba ulitiwa saini hotelini nje ya nchi wananchi kuhoji ikawa nongwa
 
Hapa ndo Magufuli na timu yake wanajisahau.

Wanajitahidi kuziba paa linalovuja ili hali mlango upo wazi.
 
Kwa kuanzia na Haya mengine yangekaa pembeni,tungepata tume huru.baaaasiiiii,kwa Maana tungepata viongozi tofauti tofauti ambao wangetusaidia kupata katiba bora kabisa inayoendaa na muda husika
 
Katiba inaweza kubadilishwa lakini wabunge wa ccm wakiwa wengi, ndani ya bunge hapana jipya kwenye hio katiba. Kuazia Rais,mawaziri na wabunge wote wa ccm wamejaa ufisadi. Ikitokea kubadilishwa katiba na kuwekwa kipengele cha rais ashitakiwe. Basi Mwinyi, Mkapa, Kikwete na huyu msukule wote wataishia jela kwa ufisadi walioufanya. Ndio maana hawapo tayari kuwaachia upinzani madaraka, wapo tayari kufanya mapinduzi wakijua mwisho wao hautakuwa mwema.

Ndukiiiii
 
Katiba inaweza kubadilishwa lakini wabunge wa ccm wakiwa wengi, ndani ya bunge hapana jipya kwenye hio katiba. Kuazia Rais,mawaziri na wabunge wote wa ccm wamejaa ufisadi. Ikitokea kubadilishwa katiba na kuwekwa kipengele cha rais ashitakiwe. Basi Mwinyi, Mkapa, Kikwete na huyu msukule wote wataishia jela kwa ufisadi walioufanya.

Ndukiiiii

Hapo pa na huyu msukule tu. Nmecheka mpaka mbavu zinaniuma.
 
Kwa hiyo Tuache waendelee kuiba mpaka hapo tutakapopata katiba mpya! Uzuri JF hatuonani Uso kwa Uso, vinginevyo moderators wangekuwa na wakati mgumu sana!!!
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mbaya wa watanzania ni CCM.
Najua kuwa ccm ni mbaya wa watanzania, lakini bado nasisitiza kuwa katiba hii tuliyonayo ni mbaya kuliko ccm ilivyo mbaya kwetu!

Kwanini nasema hivyo?
Katiba hii ikiendelea kuwepo sisi watanzania hatuwezi kufanya, kurekebisha kitu chochote! Lakini tukiiondoa hii na kupata mpya hasa ile iliyobeba maoni ya wananchi tunaweza kurekebisha mengi iwe ccm ipo au haipo.
Ndiyo maana nasisitiza adui namba moja ambaye watanzania wangemuondoa ni katiba hii halafu ndipo wamuondoe adui mwingine wanayemuona anajipitishapitisha karibu yao maana maadu wa maendeleo ni wengi.
 
Mku CCM ndiyo waliokwamisha Watanzania kupata Katiba mpya iliyobeba maoni na matakwa ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom