Watanzania kwanini tunapenda waimbaji wa kiume wenye sauti za kike?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,220
12,725
Ni kuwa tunaukike au ni nini? Waimbaji kama Q chief, Zed Anto, Voice Wonder, Alikiba, Diamond, sijui nani the prince, oliver ngoma, Muumin Mwijuma, Waziri Sonyo nk ndiyo wanakubalika sana. Watu wenye sauti zenye ujazo utaona hawafiki mbali kwenye fani.

Ukisikiliza nyimbo za wenzetu unakuta mwanaume anasauti imeshiba na inatoka yote. Sikiliza hata wahindi tunaowaonaga ni dhaifu. Mwanamke ndiyo anaimba sauti nyembamba ila mwanaume anatoa yote.

Sikiliza wanaoimba nyimbo za rock, mtu anaimba hadi ukumbi unatetema, sauti yote, kubwa na iko vyema. Cheki mtu kama Olomide, anaimba sauti imeshiba na anafanya poa sana.

Nini kimetupata hadi kuwa feminine kiasi hiki?
 
Mbona sio wote mzee ishu ni kuwa wanawake washakuwa wengi ulimwenguni, hivyo kupelekea kuwa na nguvu zaid kwa sasa wanawake ndo waamuzi kuwa msanii yupi anaeenda mjini yupi abaki, na kama ujuavyo wanawake wetu wanapenda kubembelezwaaaa haswa na sauti ya mtoto wa kiume ikiwa ya kumtoa nyoka pangoni.
 
Mbona sio wote mzee ishu ni kuwa wanawake washakuwa wengi ulimwenguni, hivyo kupelekea kuwa na nguvu zaid kwa sasa wanawake ndo waamuzi kuwa msanii yupi anaeenda mjini yupi abaki, na kama ujuavyo wanawake wetu wanapenda kubembelezwaaaa haswa na sauti ya mtoto wa kiume ikiwa ya kumtoa nyoka pangoni
Si inasemwa wanawake wanapenda mtu musculine!? Ila una point, ngoja waje watudadavulie zaidi.
 
Acha kutusemea wewe! Umefanya utafiti wapi kuhusu hii hoja yako? By the way, na huyo Oliver Ngoma ni Mtanzania?
 
Unamjua Michael Jackson wewe, unajua kwenye muziki hakuna aliyefikia level zake katika kupendwa na kukubalika kwa kipaji chake!! Haya sasa niambie tone yake ilikuwa vipi..... Wote akina NeYo, ChrisBrown, Justin Timberlake wotewote wasanii waliofanikiwa sana walikuwa na tone kali na laini.....
 
Unamjua Michael Jackson wewe, unajua kwenye muziki hakuna aliyefikia level zake katika kupendwa na kukubalika kwa kipaji chake!! Haya sasa niambie tone yake ilikuwa vipi..... Wote akina NeYo, ChrisBrown, Justin Timberlake wotewote wasanii waliofanikiwa sana walikuwa na tone kali na laini.....
Maiko alikuwa na sauti nyembamba sana, msikilize anavyohojiwa. Ila kwenye kuimba alikuwa anajikaza sana atokee kiume. Sikiliza ngoma kama Dirty Diana, beat it au black and white. Ukimeikiliza anavyohojiea na anavyoimba utaelewa jinsi alivyokuwa anajitahidi kukaza sauti.
 
Mkuu bila shaka wewe hujui music au mgeni kwenye hii sekta.
Kila mtu ana taste yake ya music hivyo acha kupangia watu maisha.
Kwenye music kuna vitengo mbalimbali.

Kuna aina tofauti tofauti za music na pia kwenye music kuna aina tofauti za sauti pia mfano falsetto, mezzo, soprano, chest voice, head voice, base nk.
na mwanaume haiwezekani kuimba sauti ya kike hata iweje bali mwanamke pekee ndio ataweza kuimba sauti ya kike ni boundaries ambazo haiwezekani kuvuka.

So unachofanya hapa ni kulazimisha kila mwanaume aimbe base na kila mwanamke aimbe high means mpaka hapo hujui music ndio maana nikakuita mgeni kwenye hii sekta sababu music sio sauti ya kike au ya kiume.

Pia kwenye music kila note inakuwa na sauti yake maybe high pitch or low pitch.
Sasa huwezi kwenda high pitch kwa kutumia base lazima utumie falsetto or head voice ambayo bila shaka wewe unaita ya kike.
Again hujui music.

Alafu nyimbo za wenzenu ndo zipi?
Kuna wasanii wakubwa kama
Ed Sheeran
Shawn mendes
Justin Bieber
Chris brown
John legend
Michael Jackson
James Arthur
Passenger
Maroon 5 nk
Hawa wote wanaimba aina tofauti tofauti za sauti na aina tofauti za music ila wewe utaita sauti za kike sababu hujui music.

Kingine kutoa mfano wa nyimbo za kihindi mpaka hapo ni dalili tosha hujui music vilevile.

Mkuu hii sekta ina wenyewe kama unasikiliza singeli na nyimbo za kihindi basi itakuwa ngumu kuelewa.
Nadhani wahindi ndio wanaongoza kwa kuimba hovyo.

Ilibidi uadmit hujui music ueleweshwe kuliko kuandika hii mada.
 
Jazia nyama kapitie huko ulikoanzia urudi na full-detailed post labda nitaweza kuelewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom