Watanzania kwanini hatupendi kuwajibika

tumpale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
201
0
Baadhi ya magazeti ya leo yametoa habari yanye kichwa cha habari, Mwakyembe ahujumiwa. Msingi wa habari ni kuwa kuna watu wanang'oa bolt kwenye reli na kuuza kama vyuma chakavu. Swali langu ni tunaohangaika na usafiri wa daladala ni sisi au Mwakyembe.?

Kwanini mtu anaharibu miundombinu badala ya kumchukulia hatua tunasema waziri anahujumiwa, imi nadhani haujumiwi Mwakyembe tunahujumiwa sisi. Jamani tubadilike nchi haina mwenyewe kuna haja ya kujitetea wenyewe, unakuta mtu anang'oa bolt na wewe mg'oe jino then mpeleke polisi ili aone faida ya kuwaletea adha watu wengine.
 

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,500
2,000
Ndo shida yetu, hatujui kipi chetu kipi sicho, tunadhani serikali ni ya viongozi
 

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
225
jamani kila mmoja wetu ana jukumu la kuilinda.. Sio lazima waje polisi wakasimame na bunduki pale.. kila mtu asimame kuwa mlinzi kwa mwenzake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom