Watanzania kubambikwa Katiba!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,585
Reaction score
14,903
Tanzania iko kwenye hatari ya kubambikwa katiba ambayo watu wengi hawaielewi, hawaiamini na ni katiba ya kichama.

Kwenye nchi za wenzetu kama Kenya na Uganda hatujaona watu wengi wakipinga katiba kwasababu ni katiba ya watu. Katiba haitakiwi kuwa na ubishano kama kweli ina nia njema lakini katiba ya Tanzania inakuwa kama inapelekwa na kulazimishwa hadi kiwango cha viongozi kuja na ratiba za kushinikiza ipitishwe.

Je kama katiba ni nzuri haraka za nini kwenye sheria ya nchi tena ukizingatia imepitishwa kwa ujanja unjanja tu na chama kimoja tu!
 
 
Mwaka huu mtayaongea yote lakini ukweli ni kuwa hakuna katiba yenye kumlidhisha kila mtu iliwahi kupatikana hapa duniani. Mengi ya wananchi yamezingatiwa hayo mengine mnayoyapigania sio ya wananchi bali ni ya viongozi wenu wanaotafuta fursa za kutawala nchi.

Tunajua povu lote mnalotoa hakuna kingine kinachowahangaisha zaidi ya kutugawa na sera zenu za kibaguzi za kuongeza idadi ya serikali 3. Hilo tu ndo linawatoa povu mpaka kesho wala hakuna cha maslahi ya wananchi wala nini....
 
Katiba pendekezwa inasema Rais hashitakiwi hata akistaafu, pia wateule wake hawashitakiwi mpaka mkurugenzi wa mashtaka atoe ruhusa, kwa kifupi kwa upande wa Utawala haina tofauti na ya sasa. Watawala wameendelea kuwa untouchable
 

Vp kuhusu uwazi na uwajibikaji? Vipi kuhusu mawaziri na spika kutokuwa wabunge? Vp kuhusu wananchi kuwawajibisha wabunge? Je kuhusu wabunge kumiliki account nje? Kuhusu ukomo wa uongozi? Nk. Hvyo vyote ni kwa maslahi ya Ukawa? Mtanzania usitumike vibaya kwa kupewa posho za bure! Leo unajiona uko sahihi lakn hyo posho hataipata mjukuu wako! Leo unachoona kinakufavor kesho kinaweza kikawa kinyume chake!! CCM haiwakomoi wapinzan bali hata wanachama wake!! Acheni ushabiki usio na tija!!! Kuna cku CCM watakuwa wapinzani na hzo sheria mnazotunga kuwabana wapinzani zitawahukum
 


Hiyo ni kati a ccm i alinda maslahi ya watawala na familia zao na si watanzania
 
unaweza kuandaa sumu kwa lengo la kumua mama wakambo ikamua mamako mazazi mfikirie miaka 50 ijayo sio mnafikiria matumbo yenu na familia zenu
 
Sioni hekima yoyote ya kuamua ku omit matakwa muhimu wanayotaka wananchi na kubambika kinga za watawala kwenye katiba kwa kisingizio katiba haiwezi kukidhi mahitaji yote. Do the best if you are not able stay aside!. Kuna haja gani ya kuandika katiba kijanja na kuipitisha kwa mabavu huku kwa makusudi mkiondoa masuala muhimu kwa wananchi kwa kisingizio kwamba hakuna katiba inakidhigi mambo yote?

Kama katiba imekidhi mahitaji ya wananchi walio wengi, si muwaache wasome wajadili washauriane halafu wayaone hayo mazuri mnayoyasema ili waipigie kura ya ndiyo?

Mna hofu gani hadi kuanza kusema "atakaye ipigia kura ya hapana arudishe kadi ya cc..".

Mara Zakia apigia zanzibar,

Mara kura za merehemu,
Mara katikba inapitishwa kwa mtutu wa bunduki. Hii ni katiba ya wapi mnayowazalimishia wananchi na kuwa singizia wanaipenda?

Kama ni kweli ni nzuri, kwa nini mnatumia nguvu kubwa sana kuwalazimisha watu waipigie kura ya ndiyo?

Bunduki za nini ?

Shame on you the witches!.



 
 
Katiba kama chaguzi za mitaa 55% kwa 45% tumeona wapi hii!! Kenya, Uganda ilikuwaje kwa wanaosema duniani ndiyo ilivyo! lol
 
Hiyo katiba inawalinda prof baba lizi na chama chake haina manufaa kwa wanyonge anaeshabikia hiyo katiba anamaslahi nayo huenda ana mjomba,baba,shangazi,au kaka ambao ni mafisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…