Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Ni kuhusu Ml.Kili, kwa hali ya kawaida kwa kuwa Ml.Kili uko mpakani kabisa mwa Kenya na TZ yetu, ilipaswa tuugawane yaani sehemu iwe Kenya na sehemu iwe kwetu na hii ni international law na ndicho tunachokipigania kwenye Ziwa Malawi/Nyasa, sasa hapa tumependelewa na 100% ya Ml.Kili umewekwa kwetu Kijiografia lkn bado Mkenya anayeishi chini ya Ml.Kili lkn ametokea kuwa nje ya mpaka akipiga picha ya Ml.Kili tunatoka povu tunataka tumkataze, hivi sisi tuna akili kweli?
Hivi Mtz anayeishi Songea, MT au sijui Manyoni ana haki ya Ml.Kili kumzidi Mkenya Mmasai aliyezaliwa chini ya Ml. huko Loitoki toki?
Hakuna nchi Dunia hii iliyopata bahati kama yetu kwenye hili swala, Nchi zote zote Duniani kama mali ya asili ikiwa mpakani basi siku zote kwa kutumia Sheria ya Kimataifa hugawanywa baina ya majirani kama vile ilivyofanywa Ziwa Nyanza, Tanganyika, Mto Ruvuma, Kagera hata Ml. Himaya unamilikiwa na nchi zilizozungukwa na Mlima huo!
Lakini cha ajabu sisi Sheria ya Kimataifa ilitusahau ikatupendelea lkn bado hata kuwapa haki Wakenya ambao kwa miaka yote kabla ya mpaka wa Wazungu wamekuwa wakiishi chini ya Ml.Kili hata kupiga picha tu tunalalamika, ingawaje hakuna binadamu yoyote anayeweza kupanda Ml.Kili bila kuingia JMTZ, sasa kwa nini tunakuwa kama watoto namna hii?
Kwa nini mnataka kuamsha mambo ambayo yamelala? Hivi mnajua kwamba wakazi wa Kenya waishio chini ya Ml.Kili wanaweza kufungua kesi kudai haki yao kuwa na Ml.Kili na kesi ikasikilizwa? Acheni mambo ya kitoto, kama mtu anataka kupiga picha Mlima mwacheni, kama anapenda kumuita mtoto wake Ml.Kili mwacheni lkn akitaka kupanda ni lazima aje kwetu na kulipia kwetu, sasa mkianza kuwakataza hata watu kupiga picha wataanza kuhoji, na huu uwezekano upo Mpaka unaweza hata kuchorwa tena kwa maana wana hoja, kama vile sisi tulivyo na hoja kwenye Ziwa Malawi /Nyasa!