Uchumi wa kanda ya ziwa ulijengwa katika biashara ya Pamba kwani kimsingi kanda ya ziwa ina mvua chache na pamba hustawi katika hali hii ya hewa.
Sio lowassa wala Magufuli hakuna anayezungumzia kufufua zao la pamba na kuweka usimamizi thabiti wa zao hili.
Wakati wa mkoloni pamba iliitwa ''white gold'' Tanganyika ilikuwa moja ya nchi wazalishaji wakubwa wa pamba duniani.
Leo hii stoo za pamba zimekuwa makanisa ya walokole na kumbi za video.
Kiwanda cha kasamwa kimegeuka kambi ya FFU. Makampuni ya kununua pamba ya copkot carlgil nyanza shirecu hayapo tena.
Vijana hawalimi tena pamba wanaendesha bodaboda na kupiga debe stendi.
Akija Lowassa mpo akija Magufuli mpo wala hamueleweki, mumekuwa majuha kuliko kalumekenge.
Mnadhani munawakomoa kumbe A na B zote sawa. Munaahidiwa kujengewa viwanda wakati hata umeme wa kumulikia shuka hakuna ila nasikia munajengewa vya kusindika ngozi za ng'ombe.
Munauza mashamba ya baba zenu munanunua bodaboda nazo haziwatoi ngoja muone mtaelewa somo tu.