Elections 2010 watani wamepagawa, sasa wanatapatapa

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
CHADEMA wameteua, Dakta slaa ulingoni,
CCM kuwatungua, kuwatoa mjengoni,
Uteuzi ulotulia, kama maji mtungini
Watani wamepagawa, sasa wanatapatapa

Slaa chaguo poa, tutakavyo kutimia,
Hakuna wa kutania, wala pua kuitia,
Kazi kwetu kuamua, Oktoba yakaribia,
Kura zote kwa SLAA, ili tupate raha.

Kura zote kwa Slaa, ili tupate raha,
Nchi kaipigania, bila kuwa na staha,
Na mengi katuambia, hakujali majeraha
SLAA chaguo la leo, kwa faida ya milele.

Kumbukeni wajameni, ni yeye alisimama,
Macho yenu fungueni, mwembe yanga kalalama
Yanachotwa mabenkini, mambo huko si salama,
Bila yeye kukemea, mapesa karibu kwisha

Akaenda migodini, akazipiga kelele
Tuachieni madini, msiyapigie misele
Mgawo uwe makini , hatutapiga kelele
Serikali ikabaini,asemacho ni bayana
.

Kama tukipiga kura , SLAA kumkubali,
Tutapata barabara, shule na maji kweli
Yeye atatupa kula, kusaza ugali na wali,
Tumchague Slaa, kama twahitaji raha.


 
Sikujua wasokile nao wanajua kupamga vina, hongera LIFUMU!!! Ndio maana nimekugongea THANKS.
 
Sikujua wasokile nao wanajua kupamga vina, hongera LIFUMU!!! Ndio maana nimekugongea THANKS.

Wasokile nao wamo kwa vina si unajua tena wasokile ni watu wa pwani ( matema beach ). Shukrani kwa thanks
 
Back
Top Bottom