Tetesi: Watangazaji wa kike TBC wagoma baada ya kutakiwa kuvua Hijabu zao wakati wa kutangaza

Ebale

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
943
1,683
(NIMEIKUTA SEHEMU HII MWENYE UHAKIKA ATUJULISHE ZAIDI)

TAFADHALI KWA WAISLAM NA WAPENDA HAKI TUFUATILIE HILI KUJUA UHALISIA WAKE.

Kuna taarifa kua watangazaji wa kike Waislam wa TBC TV wamegoma baada ya uongozi kuwataka kuvua hijab wanapotangaza.

Ieleweke ya kuwa wengi wao hupenda kuvaa hijab hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Taarifa zinadai kesho asubuhi kuna kikao kujua hatma yao.

TBC TV ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zinazotokana na wananchi wa Tanzania ambao Waislam ni sehemu ya walipa kodi.

Ikithibiti hivyo itaonesha ni namna gani nchi zetu zinakoelekea, asiyejisitiri anaheshimika na anaejisitiri anatakiwa kuvua sitara yake..
 
Kama ni kweli,Jana nilimwona Asha Haji katupia hijab nyekundu.Kiukweli alikua hajapendeza kabisa, na huenda kuna watu walitoa taarifa uongozi wa TBC, kwani aliifunga ka mtu ambaye hajui inafungwaje na kuvaliwaje.

Nadhani inabidi Zuhra Yunus apewe mchongo wa kuwafundisha jinsi ya kuifunga. kwani hata tai sio kila mtu anajua kuifunga.
 
kama ni kweli ni makosa makubwa kwani hijab ni vazi lenye heshima na la kawaida kabisa cha msingi lifungwe vizuri tu.
 
Huwa nawashangaa sana hawa waislamu ambao ikifika mwezi mtukufu ndio wanajidai wanashika dini na kutaka kila mtu anataka awaone wao kuwa ni waislam. Huu ni ushenzi wa hali ya juu, kama wewe ni mwislamu kweli mbna usiuonyeshe uislamu wako siku zote? Ni unafki mbele za allah, wakatazwe kabisa kuvaa na ikiwezekana wafukuzwe kazi
 
TBC siyo peace tv wala TV Imaan..waende huko kama wanatamani hayo mavazi...watuondolee udini wao mashetwani hao...hata TVZ wanaweza kuhamia huko...don't bother us
Uislam ni dini safi na isiyopenda ugomvi ila maneno kama haya ndo husababisha hasira na chuki,leo nimekuambia kistaarabu acha hayo maneno yako,usiwachokoze watu ambao hataki uchokozin
 
uchonganishi tu ......maana hamkosagi la kuongea kila siku nyinyi tu.....kulalamika weeeeee........
 
Back
Top Bottom