Watanganyika tumelogwa na nani? CCM au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanganyika tumelogwa na nani? CCM au?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tutor B, Dec 2, 2011.

 1. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Watanganyika tumelogwa na nani? CCM au?

  Baada ya kujiuliza swali hilo; nawashauri watanganyika wenzagu tufumbuke katika hili suala la katiba mpya ya Tanganyika kwanza na katiba ya Muungano baadaye.

  Katiba mpya tunayoitaka siyo yenye mlengo wa zamani; tunahitaji katiba mpya ya Tanganyika. Huwa najiuliza sana maswali mengi kuhusu mtu mzima kushindwa kufikiri ipasavyo. Kwa wale waliogusa hesabu, kimsingi chunguza mfano huu mdogo wa hesabu; 1 + 1 = 2
  Moja (1) ni namba inayojitegemea, moja (1) nyingine ni namba pia inayojitegemea; ili kuwa na nguvu moja; namba hizi zinaungana na kuunda namba nyingine; mbili (2) ambayo nayo pia ina uthamani wake unaotegemea msingi wa hizo mamba za awali zilizoungana. Kwa mfano mdogo huo; nirudi kwenye hali halisi ya Tanzania. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni zao la nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar. Nchi hizi mbili kabla ya kuungana zilikuwa na uthamani wake kila moja kama nchi. Kulikiwa na viongozi, katiba, bendera na kila kitu kinachoitambulisha nchi kama nchi. Zilipoungana zilipaswa kuachana na misimamo yao ya awali na kuanza safari mpya kama kitu kimoja. Jambo hilo halikuwa hivyo; badala yake mwenye ardhi kubwa na idadi kubwa ya raia (Tanganyika) akawa kubwa jinga na kutaka kuimeza ardhi ndogo (Zanzibar). Muda si muda hawa wazanzibari wamebumburuka na kuliona hilo. Hivi sasa wana rais wao, serikali yao (ya mseto), katiba yao, bendera yao, wimbo wa taifa lao, timu ya taifa lao, wana mawaziri wao, wabunge wao n.k Kwa upande wa pili; hawa wa Tanganyika waliuza kila kitu ugenini (kwenye muungano); hawana chao binafsi. Tanganyika haina rais, haina mawaziri, haina katiba, haina bendera, haina chochote cha kwake; kila kitu kimepelekwa kwenye muungano; hii ni akili au matope?

  Pendekezo langu kwa watanganyika ni kuliangalia jambo hili kwa umakini na kulifikiria kwa undani; baada ya hapo tulifanyie kazi. Kazi ya kwanza ni kutengeneza katiba ya Tanganyika ambayo watanganyika peke yao ndo wahusike kwenye mchakato wa kuiunda hiyo katiba. Kwa kumbukumbu yangu ni kwamba Zanziba walipoingia kwenye mchakato wa kutengeneza katiba yao mpya; watanganyika hatukuhusishwa hata kwa mawazo. Wamefikia hatua ya kuwa na serikali ya mseto – hatujahusishwa hata kidogo. Vivyo hivyo nasi wakati tunaamua mambo yetu tusiwahusishe; wawe wasikilizaji tu kama sisi tulivyokuwa tukipata habari kwenye media mbalimbali.

  Tukishajipanga katika utambulisho wa utanganyika ndo sasa tuangalie ni kwa namna gani tunaweza kujadili mambo ya Muungano wenye maslahi kwa nchi zote mbili wanachama wa Muungano. Vinginevyo majambazi yataendelea kutuendesha namna yanavyotaka yakiwa na uongozi wa chama cha majambazi. Tutaendelea kuwa matonya wa kimataifa, tutaendelea kuuawa na maharamia then wanapata msamaha wa rais wa Muungano ambaye hana huruma na watanganyika; yeye la muhimu kwake ni Muungano tu! pamoja kuwakumbatia mafisadi.

  Namalizia kama ifuatavyo:-
  Uendawazimu ni kurudia jambo mara nyingi kwa kutegemea mabadiliko tofauti.
  Jambo la utanganyika, katiba, maendeleo na mageuzi yamerudiwa mara nyingi, tubadilike tusije – onekana wendawazimu.

  Nilikuwa mdogo na sasa ni Mkubwa; sikuwahi kuona mwenye haki akiomba mkate!
  Miaka 50 ya uhuru ni ukubwa tosha lakini bado tunaombaomba; ni ishara tosha kuwa tumepoteza haki yetu ya utanganyika kwenye Muungano.

  Ukimuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa!
  Wewe uliye juu; unayefikiri ulijiweka huko juu, saa ya kukushusha kuko karibu sana! Aliyejuu anafuatwa huko huko na kubwagwa chini! SAA YA UKOMBOZI NI SASA
   
 2. baina

  baina JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sitaki kumuona kikwete akijifanya eti yeye ni mgeni rasmi siku ya uhuru wa tanganyika kwasababu yeye ni rais wa tanzania na si tanganyika, yeye hataki tanganyika iwepo lakini anashadadia mambo ya yake.
   
 3. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Tanganyika hatuna rais na itanishangaza sana siku hiyo nani atawakaribisha wageni waalikwa kwenye sherehe hizo, Wa zanzibar ni kama baba mdogo, JK ni kama msimamizi wa mirathi, Tanganyika nani msimamizi wetu!?
   
 4. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wasimsmizi ni majini yanayomlinda mkuu; chanzo kiko katika kale kamoto kanakokimbizwa kila mwaka na sasa kanapelekwa juu ya mlima......!!!!!!!!!
   
 5. s

  semako Senior Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sina tatizo nijualo ni kwamba,mimi ni Mtanganyika tu piga uaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,876
  Trophy Points: 280
  nikuulize swali?

  Unamfahamu Nyerere kama nani?
   
 7. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Namfahamu kama Rais wa kwanza wa Tanganyika,
  Baadaye aligeuka na kuwa rais wa kwanza wa Tanzania yenye utata hadi sasa.
   
 8. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa kuliona hilo ndg yangu, tufanyeje kuiridisha Tanganyika yetu?
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Sikumbiki ni nani alonikosoa kuhusu mfano wa hesabu ndogo lakini nilichotaka ni kuwafanya wasomaji wanielewe kirahisi hata kama walifeli mathematics. Nashukuru kwa kuchambua kwa undani zaidi kuhusu hili
   
 10. T

  Taso JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Hivi maoni yakisema, na Tume ya Katiba ikashauri na ikapitishwa, kwamba tuwe na serikali tatu na ikawa hivyo kwenye katiba mpya, ndio kusema tutakaa chini tena kuanza mchakato mpya wa kuandika Katiba ya Tanganyika? Hivi sisi ni wazima kweli? Ilitakiwa kwanza lipigwe referendum sasa hivi, je tunataka "Tanzania" ngapi? Halafu ndio tuanze huo mchakato wa kuandika hizo katiba.
   
Loading...