Watakiwa kujiunga na kusikiliza sera za CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watakiwa kujiunga na kusikiliza sera za CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Mar 29, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WATAKIWA KUJIUNGA NA KUSIKILIZA SERA ZA CHADEMA

  na Stephano Mango, Songea

  VIJANA nchini wametakiwa kuhudhuria kwa wingi mikutano na maandamano yatakayoitishwa na Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) wakati wowote katika maeneo yao ili waweze kuzisikiliza sera na mikakati ya chama hicho katika kuwakomboa watanzania.
  Wito huo ulitolewa jana na mwasisi wa Kampeni ya Washa Taa Mchana Taifa na mhamasishaji wa chama hicho, Dk. Grayson Nyakarungu, alipokuwa akiwahutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliotanguliwa na maandamano makubwa kutoka katika ofisi za chama hicho Mfaranyaki kupitia mjini hadi Majengo Stend ya Maroli ambako mkutano ulifanyika.
  Dk. Nyakarungu alisema kuwa taifa lolote duniani haliwezi kuendelea bila kutegemea nguvu kazi ya vijana katika harakati za kuleta maendeleo kwenye nchi husika lakini cha kushangaza serikali ya Tanzania imelitelekeza kundi hilo muhimu na kuwaacha vijana wakihangaika bila msaada wowote.
  Alisema kuwa muda umefika vijana nchini kujitokeza kwenye mikutano ya CHADEMA na kusikiliza kwa makini sera na mikakati imara ya yenye lengo la kuiondoa Tanzania hapa ilipo na kuipeleka kwenye neema zaidi kwa maslahi ya Watanzania wote.
  “CHADEMA ni chama makini ambacho watanzania wanapaswa kujiunga nacho kwani ndicho chama chenye dhamira ya dhati ya kuwakomboa watanzania na kuwapeleka kwenye neema kupitia rasilimali tulizojaliwa kuwa nazo nchini mwetu,” aliongeza Nyakarungu.
  Alieleza zaidi kuwa ni miaka 50 sasa ya uhuru wananchi ni maskini kwani serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeshindwa kuzilinda na kuzitumia vizuri rasilimali zilizopo nchini kwa manufaa ya watanzania wote badala yake imejikita zaidi katika kuzilinda sera mbovu za uwekezaji na kuingia mikataba mibovu katika rasilimali za umma.
  Awali mratibu wa kampeni ya washa taa mchana mkoani Ruvuma Likapo Bakari alisema kuwa vikao vingi vya kuliujumu taifa hili vinafanywa mcha na watu waliopewa dhamana ya kuwaongoza watanzania na kuzitunza rasilimali za nchi kwa maslahi ya taifa ndio maana tumewasha taa mchana ili iweze kuwamulika na kuonekana machoni mwa watanzania ili waweze kuchukuliwa hatua madhubuti kwa kutumia nguvu ya umma.
  Bakari alisema kuwa taa hiyo imewashwa ili iwasaidie watanzania kuona rasilimali zilizopo nchini kama zinatumika ipasavyo kwa maslahi ya watanzania pia iwaangazie watu wenye matatizo mbalimbali ambayo wamesababishiwa kwa makusudi na serikali yao ili wapate matumaini ya ukombozi kupitia CHADEMA na kwamba taa hiyo itapelekwa nchi nzima na vijana wa CHADEMA wa vyuo vikuu ambao wana dhamira ya dhati ya kulikomboa taifa letu

  Redmarked:

  MY OPINION:TUWAUNGE MKONO HAWA WAPAMBANAJI TUWEZE KURUDISHA HESHIMA YA TANZANIA KAMA NCHI YENYE RASILIMALI YA KUJIENDESHA BADALA YAKE TUMEKUWA OMBAOMBA.

  Nawakilisha kwa niaba ya :Stephano Mango, Songea


   
 2. i

  ibange JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Big up!
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  duh .... washa taa mchana .... hii ni operesheni mpya ...?
   
 4. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha taa iwashwe mchana, hakuna la ajabu, kwani mwenge mmewahi kuona ukiwashwa usiku?
   
Loading...