Wahenga walisema, "kusoma sio kazi, kazi kupata kazi".Fact, huwez somea ubwana shamba eti ukauze lambalamba hiyo elimu ya ubwana shamba itakuwa imo kweli ? Mwenyewe ni mhanga wa ajira lkn mpaka najilaumu Kwa nn nisingeishia tu form four maana leo naona niliomaliza nao form four wanamaendeleo kupita mm na wengine wananidharau nakuniambia ulisoma nn sasa ona unaanza mwanzo sisi tulishakupta sana
Mkuu, kuna zile ajira za kubeba madishi ya Jambo na Cello, nikuunganishe?
Umechangia vyema ,sijajua kama JF kuna watu wenye akili kubwa kama ww!Mawazo kama haya nayasikia hata kwa viongozi kadhaa na baadhi wenye ajira, sasa watu wanasoma Chuo ili iweje kama hawawezi kuja kutumika katika nafasi ambazo wana ujuzi nazo? mawazo kama haya yanapelekea kukatisha tamaa ambao wapo ngazi za chini za kielimu.
Ni sahihi kabisa kama mtu atatafuta ajira isiyo ya taaluma yake kama tu itakuwa ajira ya ziada kwa ajili ya kuongeza kipato, huko kwa wenzetu hizo ajira unazozisema wanazifanya watu wenye elimu za kawaida tu na kama ajira za ziada. Mtafuta ajira anayo haki ya kuchagua kazi kwasababu sio kila kazi ana ujuzi nayo, na anayo sababu ya kutafuta kazi ya ujuzi wake ili awe na tija zaidi kwa mwajiri wake.
Tofauti na hapo hizi stori za kazi yeyote tunakubali kama taifa tumeshindwa kukuna vichwa jinsi ya kuwatafutia watu wetu ajira kulingana na taaluma zao ili wawe na tija kwa taifa, Swali la kujiuliza kwanini mtu Asome uhasibu, udaktari, Uhandisi, Uanasheria halafu badala ya kuutumia ujuzi wake awe muuza chipsi? Kwa nini Chipsi zisiuzwe na waliosomea Nutrition na mambo ya Chakula? Moja ya jawabu Taifa letu hatuheshimu Ujuzi ndo maana kuna vitu tunavichukulia poa tukiamini havihitaji Elimu lakini si kweli, Wenzetu Salon zinasomewa kabisa, upishi ndio usiseme
Mkuu nikuhakikishie haupo wewe pekee katika kundi hili ni wengi, hii hali inatokea sababu wenye dhamana ya kufanya maamuzi ya uelekeo wa Taifa letu wengi hawaguswi na haya ambayo wengi yanawaumiza, tunazungumzia viongozi ambao wao wanapokea mishahara ya kutosha, wanapeana marupurupu na pensheni zilizonona, Watoto wao wanasoma shule nzuri na vyuo bora kabisa wanawahakikishia nafasi za ajira kwenye mashirika ya umma au makampuni makubwa ambayo wana ushawishi, Mwenye shibe hamjui mwenye njaa, lakini laiti hili swala lingekuwa linatukumba wote hakika hali isingekuwa hivi. Nikupe mfano tuna uhitaji mkubwa sana wa Madaktari, Wahandisi, Walimu, Manesi, Wanasheria, Wahasibu kila aina ya wataalamu serikali ina mapungufu, Serikali haitaki kuajiri sababu haina mishahara ya kuwalipa, Mwalimu Mmoja Mshahara wake ni kuanzia laki 7, Mhandisi laki 9, Daktari 1.4m Lakini Tuna wabunge Zaidi ya 350, Mbunge Mmoja Mshahara na Marupupu yake anapokea takribani 11m, Hivi tungeshusha hayo marupupu hata mpaka 5m Tungeajiri wataalamu wangapi? Mbunge anakiinua Mgongo cha zaidi ya milioni 350 kwa kufanya kazi ya kuwakilisha wananchi kwa Miaka 5 tu, Mwalimu aliyedumu katika utumishi kwa zaidi ya Miaka 35 hawezi kufikisha Pensheni ya Milion 200,major mwendwa, Fact, huwez somea ubwana shamba eti ukauze lambalamba hiyo elimu ya ubwana shamba itakuwa imo kweli ? Mwenyewe ni mhanga wa ajira lkn mpaka najilaumu Kwa nn nisingeishia tu form four maana leo naona niliomaliza nao form four wanamaendeleo kupita mm na wengine wananidharau nakuniambia ulisoma nn sasa ona unaanza mwanzo sisi tulishakupta sana