Wanajamii nahitaji msaada wenu kidogo…Mimi hapa ninapokaa kwa mbele kuna kanyumba ka uswahili sasa muda wa kufturu umefika nikaletewa uji,kuletewa nikaona aibu ikabidi nyinwe tu maana ningeonekana vipi kwa watu au labda na ringa…ule uji nimekunywa kama robo hivi kikombe,mwingine nimeingia home nikamwaga,na nikaenda chooni kutapika nikahakikisha uji wote umeisha…Swali langu,je kama mtu alikuwa na nia mbaya na mimi kupitia hicho kiwango kidogo cha uji anaweza nidhulu au nilivyojitapisha bado naweza dhulika? Wakuu nipeni muongozo,nakumbuka kwetu niliambiwa usipewe vitu vya kula kula hasa kwa watu usiowaamini