Ndugu zangu Watanzania awali ya yote niwatakie Waislam wote Nchini IDD -MUBARAK. Ndugu zangu Watanzania naomba tutambue kuwa hii Nchi ni yetu sote na hakuna mtu yeyote awaye, kikundi au taasisi inayoweza kusema kuwa hii Nchi ni mali yake! Kwa msingi huo nasema kila mtu anayo haki kuona mustakabali mwema wa Nchi hii kwani maisha yake yanategemea uwepo mwema wa Nchi hii!
Nasema mapema kabisa kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 tulimpata Rais wetu mpendwa Dr.John Pombe Joseph Magufuli,Mtanzania na Mtu mwenye mapenzi makubwa na Nchi hii .
Ni mtu ambaye kazi zake tangu akiwa Waziri zimeonekana kwa kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na Nchi hii! Pamoja na mazuri ya Mhe.Rais wetu lazima tukubali kabisa kuwa yeye si MALAIKA wala MUNGU,yeye ni binadamu na ana mapungufu yake kama walivyo binadamu wengine! Mhe.Rais wetu na sisi Watanzania lazima tutambue kuwa Nchi hii (kwa maana ya Eneo na Ardhi) imekuwepo kwa muda mrefu na kumekuwepo na jitihada nyingi tangu enzi za Babu zetu, Nyerere,Mwinyi,Mkapa ,Kikwete na sasa Magufuli.Kila zama zilikuwa /zimekuwa na changamoto zake. Hivyobasi Mhe. Rais wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli lazima atambue kuwa jitihada zozote za kuendeleza Nchi hii lazima ziwe ni muendelezo katika mafanikio tuliyokwisha yapata na pale ambapo hatujapata mafanikio kazi yake sasa iwe ni kutafuta mafanikio hayo!
Haya ni maeneo ambayo kwa mtazamo wangu kwa kuanzia Mhe.Rais wetu na wataalam /washauri wake wanapaswa kuyaangalia upya ili wasiturudishe nyuma!
1. Demokrasia na Uhuru katika upashanaji wa habari (sitatoa maelezo hapa).
2. Uchumi ambao msingi wake unaeleweka (sasa Dunia ina uchumi unaozingatia nguvu ya soko na kinyume chake ni kujidanganya).
3.Kutenganisha kazi za kitaalam na zile za kisiasa! (Rejea kuokota watu vijiweni na kuwateua kuwa Makatibu Wakuu Wizarani na Makatibu tawala wa Mikoa na Wilaya).