Wasyria watangaza uungaji mkono kwa Hizbullah

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,193
10,681
4bk3d29f3035724n9d_620C350.jpg

Raia wa maeneo kadhaa ya Syria wamefanya maandamano wakitangaza uungaji mkono wao kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon.

Wakazi wa miji ya Al-Fu'ah na Kufriya kaskazini mwa jimbo la Idlib nchini Syria na ambao wamekuwa wakizingirwa na makundi ya kigaidi kwa muda mrefu sasa, walifanya maandamano hayo hapo jana, ambapo sanjari na kulaani hatua za Baraza la Ghuba ya Uajemi za kuitaja harakati ya Hizbullah kuwa ya kigaidi, wameunga mkono pia nafasi ya harakati hiyo ya Kiislamu katika kupambana na maadui wa Uislamu ikiwemo Israel na makundi ya kigaidi. Waandamanaji hao sanjari na kutoa nara za kuunga mkono nafasi chanya ya kimapambano ya Hizbullah katika kukabiliana na utawala haramu wa Kizayuni na kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina na kadhalika mapambano yake dhidi ya wanachama wa makundi ya kigaidi na kitakfiri yanayotumikia maslahi ya Marekani na utawala wa Kizayuni, wamesisitiza udharura wa kuongezwa juhudi zaidi za kujitolea za harakati hiyo ya Hizbullah. Jumatano iliyopita, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linaloundwa na nchi za Saudia, Oman, Bahrain, Kuwait, Qatar na Imarat liliweka harakati ya Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi, hatua ambayo mbali na kukosolewa vikali na pande mbalimbali, imetajwa kuwa imechukuliwa kufuatia mashinikizo ya serikali ya Washington na utawala wa Kizayuni. Mbali na Syria, nchi za Lebanon, Iraq, Algeria na Tunisia zimepinga vikali hatua hiyo ya PGCC na kutangaza wazi kuwa hazitoheshimu maamuzi ya baraza hilo kuihusu harakati hiyo ya Kiislamu.




Maandiko yanayofanana




Ufeministi

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (22)
Katika vipindi vilivyotangulia tulinukuu maneno ya baadhi ya wataalamu waliosema kuwa japokuwa ufeministi umekuwa na baadhi ya matunda katika uwanja …

Hadithi

Hadithi ya Uongofu (33)
Assalaamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. Katika …

Afya

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha
Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

na wasomaji wa mtandao …

WahtsApp-Logo-Radio-1.jpg




Jiunge Nasi katika Facebook




Zilizotembelewa zaidi
Polls
Unasemaje kuhusu maafikiano ya amani nchini Syria
Nina matumaini Sina matumaini Sina la kusema
 
Back
Top Bottom