VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Komredi Stephen Wasira nakutafuta. Hata Lumumba sikuoni siku hizi. Nakutafuta nikuombe utoe utabiri mwingine. Ule naona umekwenda kinyume. Umewaimarisha badala ya kuwasambaratisha. Najua nawe una karama za kiutabiri. Komredi Wasira, fanya mambo. Redio zitatangaza na magazeti kuandika kwa wingi. Safari hii utabiri wako utatimia. Please, show yourself for CCM!
Komredi Wasira, ni wewe uliyetabiri kuwa CHADEMA itasambaratika na kufa miaka ya nyuma. Makada walipa-ada tukakushangilia kwa kutusaidia. Kwa kuwaombea mabaya (kiutabiri) wapinzani wetu. Tukakuona kama mkombozi wa chama na hata kupewa airtime ya kutosha kwenye Mchakato wa Katiba mpya na hata kwenye kuandaa Ilani ya CCM ya mwaka huu kama Mwenyekiti wa Ilani. Tukakuona kuwa wewe ni kiboko ya wapinzani hasa CHADEMA.
Uko wapi Komredi? Nakutafuta kweli kweli. Najua umeshashinda kumkwamisha Bulaya asigombee Jimbo nawe kule Bunda. Bulaya angepitishwa kugombea, pasingetosha. Lakini,weledi wako kisiasa umemkwamisha Bulaya kisasa bila anasa wala mikasa. Ikaonekana amekataliwa na wanaCHADEMA wenyewe. Hiyo imekaa safi. Bulaya kwisha kazi yake. Labda abaki kama Mbunge wa Vitu...hapana ni viti maalum. U wapi Komredi?
CHADEMA wamemea na kuenea. Wameungana na wenzao na kuunda UKAWA na sasa wana power. Tafadhali jitokeze Komredi utabiri tena kuhusu CHADEMA na hata UKAWA. Harakisha kwakuwa sasa hali inatisha na inatuambia pisha. Uko wapi Komredi Wasira utabiri tena?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam