Wassira: Tumeongeza Muda Kidogo, Chadema Itakufa Kabla ya Pasaka

Wassira: Tumeongeza Muda Kidogo, Chadema Itakufa Kabla ya Pasaka

Status
Not open for further replies.

MKAMA6

Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
65
Reaction score
110
Akihojiwa na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar Es Salaam jana Wakati wa Sherehe ya Mabalozi wa Nchi za nje hapa Nchini Iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Kwa ajili Kuukaribisha Mwaka Mpya.

Pamoja na Mambo mengine ya Kitaifa aliyohojiwa Mhe.Wassira na Waandishi wa Habari, Pia aliulizwa Swali na Mwandishi wa Habari wa Kituo Cha ITV Bi.Ufoo Saro Kwamba "Mhe.Waziri Vipi Kuhusu Kauli yako Uliyoitoa Juu ya CHADEMA Kufa/Kusambaratika Kabla ya January Mwaka huu 2014!?...

Wassira:"Swala la CHADEMA Kufa liko palepale, I think Kabla ya Pasaka hii Inayofuata, Chadema haitakuwa hai...haikuweza Kufa Kwa Sababu Kuna Mambo hayakwenda Vizuri Mwishoni mwa Mwaka jana, Ila Kuweni na Subira tu... alisema Wassira. Katika Mahojiano hayo, Mhe. Wassira pia amepata fursa ya Kuuzungumzia Mgogoro Uliopo Kati ya Mbunge Zitto Kabwe na Chama Chake, Mhe. Wassira amesema "Chadema Wanajiita Chama Makini lakini Wanashindwa Kuidhibiti Mienendo ya Wanachama na Viongozi Wake tangu Awali, na hii Itawasumbua sana"

Source: Gazeti Habari Leo.
 
mmh! hii noma sasa! CHADEMA tujipange sawa sawa... Kauli hii!
 
Ewe Mungu, tunakuomba iwe kinyume chake kwa aliyetamka na maombi haya yatimie!
 
Wassira:"Swala la CHADEMA Kufa liko palepale, I think Kabla ya Pasaka hii Inayofuata, Chadema haitakuwa hai...haikuweza Kufa Kwa Sababu Kuna Mambo hayakwenda Vizuri Mwishoni mwa Mwaka jana, Ila Kuweni na Subira tu... alisema Wassira.

Hapo nilipokolezea wino naona panahitaji maswali ya kina, kuna mambo hayakwenda vizuri mwishoni mwa mwaka jana,mambo yapi hayo?
 
Amelaaniwa huyu mzee, mwenye nia mbaya ya kuiharibu tumaini la watanzania ili tembo wetu, madini yetu yachukuliwe na mafisadi wa chama chake CCM
 
naona wasira ndiye aliyetabiriwa na Yahaya junior kwamba atakufa hana hata soni anadhani nchi hii ni ya mama yake kati ya watu watakaopelekwa the Hague huyu mzee lazima awemo nitashangaa kama kurugenzi ya habari chadema wataiacha kauli yake ipite hivi hivi bila kumzaba nayo usoni
 
Ha ha ha ha ha! Kweli Zitto ni kamanda hasa, Yani kashapiga fedha za magamba, ona sasa anazidi kuyapiga kalenda tu,
ilikuwa kabla ya 2013 na sasa kayasogeza mbele eti baada ya pasaka na mwisho wa siku atayapiga tena kalenda kwamba CDM itakufa baada ya Yesu kurudi.
 
Last edited by a moderator:
ZZK alikosea fomula waliyompa.

Ha ha ha ha Mkuu tatizo tena Zitto ni mtoto wa mjini kwani anajua fika kazi aliyopewa ni ngumu sana lakini ameamua ayapige mzinga magamba.
 
Last edited by a moderator:
dah Chadema wamekorogeka., kwa majibu haya ya wasira inaonekana kuna mikakati madhubuti ndani ya CCM kuikoroga chadema na CCM sasa wameanza kufanikiwa.,
 
Kwa mtanzania makin na mzalendo ni muumini wa ccm imara na cdm imara,lakini kwa wale wanaoshabikia watu na taasisi zao ni sahihi waamini hivyo wanavyoamini.
 
Hapo nilipokolezea wino naona panahitaji maswali ya kina,kuna mambo hayakwenda vizuri mwishoni mwa mwaka jana,mambo yapi hayo?

Unajua kuna hela tulikuwa hatujamkamilishia Zitto sasa kipindi fulani akawa amesimamisha hujuma kidogo ila kwa sasa tumeshamalizana nae tunasubiri vitendo tu
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom