Katika mahojiano na Gazeti la Dira ya Mtanzania,Mbunge wa Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na uratibu) Stephen Masatu Wasira amesema kuwa ccm inao viongozi wasafi na yenyewe ni safi ndio maana imelilea Taifa katika misingi ya upendano,mshikamano,amani,utulivu na kwamba ccm inazidi kuboresha huduma na ustawi wa watu katika Taifa hili.
Wasira anasema yeye mwenyewe anajiamini kwa dhati kuwa ni msafi na mwadilifu mbele ya Taifa lake na chama chake."Kama kuna mtu anauona uchafu wangu awaeleze watanzania;asiogope wala asijifiche kusemea pembeni"
Katika mahojiano hayo,Wasira anakiri kuwa kama asingekuwa msafi Ukawa wangemmaliza maana wanamuona kuwa ni mtu anayewakera sana.Wasira anasema hao watu(Ukawa) wamejitahidi sana kumchunguza na dosari zake ili wammalize na kumnyamazisha kabisa,lakini wameshindwa kuzipata maana hazipo.
Hivi wana jf, ni kweli kuwa kiumbe huyu ni msafi kiasi hicho?