Hiki Kipindi hakina mvuto tena, karibu kila siku anawahoji viongozi wa serikali hususani waziri, makada wa CCM tu, halafu anarudia rudia kuwahoji watu wale wale tu, bado sioni maswali magumu hususani Specific Question hakuna kabisa.
Ukichunguza kwa makini utadhani mtangazaji alishaandaa maswali na kumpa muhusika kabla ya siku ya kumuhoji au Mhusika ametengeneza maswali na kumpa mtangazaji ili aje kumhoji.
Baya zaidi hicho kipindi ni recorded hivyo kinahaririwa sana kabla ya kurushwa hewani, hivyo sio realistic.