Elimu ya Uraia ndio ufunguo kwa haya yote. Ikiwa watu wetu watakuwa wamepata elimu ya uraia ya kutosha wao wenyewe watajua jinsi ya kuweza kukataa ujinga wa aina yoyote hata kama unatokea Ikulu. Kwa hiyo kazi kubwa mbele yetu tulio na mwanga kidogo ni elimu ya URAIA vijiweni, kwenye misiba, kwenye harusi, vijijini, shuleni, vyuoni na hata kwenye vituo vya kusubiri mabasi. Sema kwa anayesikia, tumia ishara kwa asiyesikia. Elekeza, elimisha, elezea ili wengi wakielewa tutaweza simamia haki sio kwa serikali hii tu, bali hata nyingine zijazo.