Wasomi, Msako Wa vyeti feki umeishia kolomije?

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
300
423
Vyeti feki na uhakiki Wa vyeti ni single ambayo iliibuka kwa kasi huku ikipigwa na karibu kila kituo cha redio za Serikali ya awamu hii.

Tena kwenye baadhi ya vituo ilienda mbali mpaka kusababisha watu kuacha kazi na wengine kukosa uhalali wa kulipwa mafao yao ilihali walishalitumikia taifa kwa muda mrefu sana.

Pasi na shaka kila mmoja mwenye uchungu na hii Nchi bila kupepesa macho lazima awe na mashaka juu ya mwenendo Wa ukaguzi Wa vyeti na ufuatiliaji Wa taarifa.

Pamoja na huu ukaguzi kulisitishwa pia maslahi ya watumishi Wa Umma .Kama upandaji Wa madaraja ,ongezeko la mishahara (increments) na baadhi ya ajira kuondolewa na wengine kufutiwa kabisa ajira. Kuna ambao walipewa barua mwaka za kupandishwa madaraja ila mpaka Leo hakuna fedha iliyoongezeka kwenye mishahara yao. Pamoja na hilo kuna ambao wanatakiwa kupandishwa mwaka huu tena mwezi huu Wa NNE sasa sijui nao watapandishwa kwa kupewa barua tu au pamoja na stahiki zao?

Serikali inatumia fedha nyingi sana kwenye suala la Elimu ,hasa Sera ya Elimu bure kuacha mianya ya watu kutumia vyeti feki itakua ni sawa na kusema Elimu yetu haina maana yoyote.

Hoja ya vyeti inakua na nguvu mno kwani ni utaratibu unaotumika tuniani kote kuhakikisha watu wote wanaopewa dhamana ya kufanya shughuli yoyote ile wana weledi Fulani kufanikishwa suala husika.

Udanganyifu kwenye Elimu umewagarimu watu wengi waliojihusisha na suala hilo.
Wengi wamepatwa na maswahibu ya kuachishwa kazi kuvuliwa vyeo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ukiwa mtu ataenda mbali zaidi na kufoji vyeti vya Elimu ikithibitika INA maana MTU huyo anatakiwa ashughulikiwe pia katika hali ile ile wanayoshughulikiwa wengine pasi kujali wadhifa au cheo chake. Ikishindikana kufanyika utaratibu Wa namna hiyo na wasomi wakakaa kimnya maana yake ni kwamba Elimu yetu haina thamani hata kidogo.

Gharama na muda unaotumika kwenye Elimu ni mkubwa mno.

Vyeti kwanza nawasilisha.
 
Tanzania nchi ya ajabu sana. Sasa wale walioachishwa kazi kwa sababu ya vyeti wanapoona mwenzao anapeta wanajisikiaje?
 
Duh kweli inasikitisha sana hii yaani ingekua ni RAIA mwingine hii ishu ya vyeti ingemletea shida sana hapa sijui ni nini kinaendelea.
 
Vyeti feki na uhakiki Wa vyeti ni single ambayo iliibuka kwa kasi huku ikipigwa na karibu kila kituo cha redio za Serikali ya awamu hii.

Tena kwenye baadhi ya vituo ilienda mbali mpaka kusababisha watu kuacha kazi na wengine kukosa uhalali wa kulipwa mafao yao ilihali walishalitumikia taifa kwa muda mrefu sana.

Pasi na shaka kila mmoja mwenye uchungu na hii Nchi bila kupepesa macho lazima awe na mashaka juu ya mwenendo Wa ukaguzi Wa vyeti na ufuatiliaji Wa taarifa.

Pamoja na huu ukaguzi kulisitishwa pia maslahi ya watumishi Wa Umma .Kama upandaji Wa madaraja ,ongezeko la mishahara (increments) na baadhi ya ajira kuondolewa na wengine kufutiwa kabisa ajira. Kuna ambao walipewa barua mwaka za kupandishwa madaraja ila mpaka Leo hakuna fedha iliyoongezeka kwenye mishahara yao. Pamoja na hilo kuna ambao wanatakiwa kupandishwa mwaka huu tena mwezi huu Wa NNE sasa sijui nao watapandishwa kwa kupewa barua tu au pamoja na stahiki zao?

Serikali inatumia fedha nyingi sana kwenye suala la Elimu ,hasa Sera ya Elimu bure kuacha mianya ya watu kutumia vyeti feki itakua ni sawa na kusema Elimu yetu haina maana yoyote.

Hoja ya vyeti inakua na nguvu mno kwani ni utaratibu unaotumika tuniani kote kuhakikisha watu wote wanaopewa dhamana ya kufanya shughuli yoyote ile wana weledi Fulani kufanikishwa suala husika.

Udanganyifu kwenye Elimu umewagarimu watu wengi waliojihusisha na suala hilo.
Wengi wamepatwa na maswahibu ya kuachishwa kazi kuvuliwa vyeo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ukiwa mtu ataenda mbali zaidi na kufoji vyeti vya Elimu ikithibitika INA maana MTU huyo anatakiwa ashughulikiwe pia katika hali ile ile wanayoshughulikiwa wengine pasi kujali wadhifa au cheo chake. Ikishindikana kufanyika utaratibu Wa namna hiyo na wasomi wakakaa kimnya maana yake ni kwamba Elimu yetu haina thamani hata kidogo.

Gharama na muda unaotumika kwenye Elimu ni mkubwa mno.

Vyeti kwanza nawasilisha.
Udhibiti wa vyeti umefutika, au unasubiri TBC itangaze?
 
Back
Top Bottom