Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa uhamiaji mkoa wa Arusha wamewakamata wahamiaji haramu 11 wakiwemo wanawake sita kutoka nchini Somalia na kuwafikisha mahakamani kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria.
Akisoma shtaka hilo namba 22 /2017 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arusha Bw Nestory Barro, mwendesha mashtaka wa serikali kutoka idara ya uhamiaji Bi Jamilla Ilomo amesema wastakiwa hao walikamatwa januari 11 mwaka huu wakiwa ndani ya nyumba ya kulala wageni inayojulikana kama Olasiti Guest House iliyopo eneo la Olasiti jijini Arusha.
Aidha mwendesha mashtaka huyo Bi Ilomo amedai kuwa watuhumiwa hao wameingia nchini kinyume na kifungu cha 28 (1) (a) (b) na (c) na kifungu cha 44(1) (2) cha sheria ya uhamiaji sura no 54 ya mwaka 2002 ilivyofanyiwa marekebisho na sheria no 8 mwaka 2015 inayokataza kuhifadhi wahamiaji haramu.
Kwa upande mwingine akizungumza nje ya mahakama hiyo mwendesha mashataka huyo ambaye pia ni mwanasheria wa idara ya uhamiaji amesema amewaonya baadhi ya wanaosaidia kuwaingiza na kuwahifadhi wahamiaji haramu sheria itachukua mkondo wake.
Hata hivyo watuhumiwa hao wote 11 baada ya kusomewa shtaka lao wamekiri na ndipo hapo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bw Nestory Barro alipowadirusha mahabusu kwa siku 14 hadi hapo februari mosi mwaka huu shauri lao litakapotajwa tena.