PreGE2025 Wasira: Viongozi wanaohubiri chuki wame wrong namba

PreGE2025 Wasira: Viongozi wanaohubiri chuki wame wrong namba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,441
Reaction score
5,238
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo watu wake wanaishi bila ya kubaguana kwa dini, rangi au kabila na kwamba hayo ni matunda yaliyotokana na kazi nzuri ya kujenga umoja na mshikamano iliyofanywa na waasisi wa taifa.

Aidha, amewataka wananchi kuwaepuka viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakihubiri kuvuruga amani, umoja na mshikamano uliojengwa na kudumu nchini tangu kuasisiwa kwake na kusema wanaofanya hivyo wamepiga ‘wrong namba’.

Ameeleza hayo leo Juni 11, 2025 alipokuwa akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi wa CCM Wilaya ya Nyasa, katika mji wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma ambako anaendelea na ziara ya kuimarisha Chama.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Tuna makabila 126 lakini tunazungumza lugha moja, sasa ukikuta mtu ana akili timamu tena ni kiongozi wa kisiasa anataka kubomoa umoja huu huyo mwambieni amekosea njia, mwambie umepiga ‘wrong namba’.

“Unajua unapiga halafu unaambiwa namba uliyopiga haipatikani. Sasa mwambie hapa ulipopiga ni namba ambayo haipatikani. Niwaambie mafanikio yetu kama Chama katika Afrika ni kuwaleta watu pamoja na wakaishi kama familia moja na msingi wa umoja wetu ndio siri ya amani yetu,” alieleza.

Screenshot 2025-06-11 214606.png
 
Wasira aache uzwazwa wake hapa Bunda ye anabagua watu wa ngapi tena bora angetulia tu kabla hatujafukua maovu yake
 
Back
Top Bottom