Wale tunaotetea matendo ya kikatili ya watawala wetu, tunafanya hivyo kwa utashi wetu kabisa au kwa maslahi ya kukidhi haja zetu? Hivi CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, CCM n.k ni miongoni mwa madhehebu ambayo kwayo tunaunganishwa na Mungu Baba hata ifike mahali sisi waamini wa dini zetu tuthubutu kuwakejeli viongozi wetu wa kiroho kwa maslahi ya VYAMA? Vyama nini hata tuviabudu kiasi hiki? What is CHADEMA, CUF n.k?
Bahati mbaya zaidi, vijana wa leo tusiojitambua na hata kujua kesho yetu tunageuka kuwa wasemaji wa serikali jiwe! (STONEY LED GOVERNMENT). Kama viongozi wetu wa kiroho wanakemea matendo ambayo ni kweli yanatokea na yapo, kwa nini tuseme wanachanganya dini na siasa? Ni akili gani hiyo kuhoji uhalali wa makemeo kwa kigezo cha wakemeaji kuwa viongozi wa dini?
Nadhani serikali isidhani ipo salama kwa kupata watetezi WANAFIKI wanaoukubali uongo kwa kuupinga ukweli ili kujipendekeza kujaza matumbo yao! Laana ya damu isiyo hatia kumwagika kwenye ardhi yetu itawalilia daima?