PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,455
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kinafuga wasiofugika kinabeba wasio bebeka,na kujaza kwenye chama wasiostahili kuwamo.huko ni kufuga matatizo"wengine wanaita kununua matatiza na kujilimbikiza shida bila sababu.
Miononi mwa waliojazwa ndani ya Chadema na ambao hawastahili kuwamo ni John Magele Shibuda,mbunge wa Maswa Mashariki. Shibuda ni abiria aliyedandiagari njiani.Aliingia kwenye chama hiki baada ya "kufukuzwa" kutoka CCM.
Akiwa CCMShibuda alivikejeli vyama vya upinzani. Alirusha vijembe kwa misemo mbalimbali. Alipoengiliwa katika mchakato wa kugombea ubunge na kukimbilia Chadema,alikipamba na kukisifu kwa sifa kedekede.
Ushindiwake wa kuingia bungeni kupitia Chadema,ulikuwa na gharama kubwa. Damu ilimwagikana roho ya mtu ilipotea. Akihutubia semina ya kujitadhimini kwa Utawala Bora Bara la Afrika
(ARPM),Shibuba alifikia hatua ya kutukana vyama vya upinzani kwa kuvifananisha na "chokoraa".Anasema vyama hivyo ni kama mtoto wa mtaani aliyekosa maleziya baba na mama.
Chama anacho kiita "machokora" kilipambana kufa au kupon ili kumnasua kutoka mahabusu alikokaa siku kadhaa akisubiri kupelekwa mahakamani kujibu mashata ya mauwaji. Hadi sasa, Shibudahajui ni kina nani waliwezesha kulipa gharama za wanasheria waliorushwa na ndege kwenda Maswa kumnasuana tuhuna za mauwaji.
Tume ya uchaguzi (NEC)ilimpa adhabu kwa kusitisha kampeni zakekwa siku kadhaa na kwa mara yakwanza Shibuda alikuwa mtiifuna myonge. Alinyenyekea mbele ya Chadema huku yeye mwenyewe akidai yuko tayari kuishi kama mfagizimakao makuu ya chamaa,kuliko kuwa mbungekupitia ccm.
Mabere Marando,mwasisi wa mageuzi nchini,akapiga mbio hadi Maswa kumtafutia ubunge Shibuda. Wakati huo Shibuda alikuwa bado anasota Mahabusu. Wakati akiwa mahabusu Shibuda alikilaani CCM na kukiona kuwa chama cha machokoraa. Alitoa kila aina ya tuhuma.Akitunana viongozi wake wakuu akiwemo liyekuwa katibu mkuu Yusuf Makamba.
Hakika siyo makamba pekee yake aliyefumuliwa mvua ya matusi,Shibuda alimtusi kila mmoja ndani ya chama hicho. Aliwahi kuwashutumu viongozi wake kwa mafumbo,na hata kuwafananisha na Nduli Idi Amin wa Uganda. wiki inayo isha,Shibuda kwa mara nyingine tena, ameomba kufutwa uanachama wa Chadema.
Ameomba kufukuzwa ndani ya chama.Ameomba avuliwe ubunge.Amesema, kwasauti ya ukali kuwa katika uchaguzi mkuu ujao atatafuta chama kingine ili kugombea ubunge, Hakuishia hapo.Amekituhumu chama hiki kuwa hakina Demokrasia.Amekivisha kilemba cha udikteta.
Zipo habari pia kwambawabunge wa chademawalipokuwa kwenyevikao vya ndanivya kuwekana sawa na kupanga mikakai ya kazi,Shibudaaliwaruka kwa maneno makali na kuwashambulia kwamba hawajui siasa" ni watoto wachanga na wanaharakati".
Yawezekana Chadema ikaendelea kulea haya? Yawezekana ikamwacha na ubunge wake?Yawezekana ikamvumilia kamaambavyo kimefanya huko nyuma? Hakika, hayo yakitendeka, chama hiki kitakuwa kinaimwa na pengine,kitakuwa kinahitaji maombi.
Kama kuna kazi nzuri ambayo makamba atasifika kwa kuifanya ndani ya CCM wakati wa uongozi wake, basi ni kumfukuza Shibuda. Aliwasumbua sana. Hivyo hivyo, Chadema sharti wafanye kama ambavyo Makamba alitenda ndani ya chama chake.Shibuda, siyo mtu wa kumuacha tena ndani ya chama hiki.
Mashitaka yake yako wazi. Amekwenda kinyume na maelekezo ya kamati kuu (CC). Hafuatimaelekezi na maagizo ya viongozi wake. nichama kilekile ambacho miaka minne iliyopita,kilimbeba na kumpa ubunge.
Chama anachokituhumu,ndicho hicho hicho ambacho kimemtia mbeleko hadi akapata ubunge.Chama anachokitukana sasa amesahau kuwa ndicho alicho kikimbilia kujifucha. Huu ni usaliti na hakika dhambi hii haina msamaha.
Anaweza kujisifu kwamba alishinda kutokana na kukubalika kwake. Lakini kwa kuwa shria haijaruhusu mgombea binafsi, asingeweza kugombea bila ya Chadema kumruhusu. Sibuda anasema hatambui UKAWA - unaoundwa na vyama vitano vya upinzani. Hatambui madai yao,hatambui kwanini wameamua kususia Bunge la katiba. Hatambui hata kama hawako bungeni! Hiki siyo kihija bali ni wehu.
Kwa maneno yake mwenyewe Shibuda amesema anachoamini yeye, ni tofauti ya sera ya chama chake, ikiwa hivyo ndivyo, nani amemtuma Shibuda kujiunga na Chadema? je, hakujua sera ya cham tangu kinaanzishwa kuwa muungano wa serikali tatu? Hivyo basi kuendelea kwake kuwa mbunge wa Chadema, hata kwa kufikiria imebaki mwaka na nusu tu,ni hatari kwa mustakabali wa chama hicho. Ataendelea vipi kuwa mbunge wa chadema wakati moyo wake hauko kwenye chama?
Nivyema basi kwa uongozi wa Chadema kuchukua hatua za harakana kumfukuza Shibuda. Kwanza si yeye mwenyewe katamka kuwa hayuko Chadema na mwakani atagombea kwa tiketi ya chama kingine? Akifukuzwa anaweza kweli kwenda Mahakamani kupinga atakuwa na hoja ipi?
Pili akibaki Chadema wakati haamini karika sera ya chama hicho, ni unafiki mwingine. Kama angekuwa ni mtumwenye ujasiri na msimamo usiotetereka, angetamka sasa hivi anajitoa Chadema na potelea mbali, Vinginevyo, ni mwanasiasa anayeonyesha woga mkubwa wa kupoteza ubunge wake na marupurupu.
Nivigumu kuamini kama Shibuda ni mwanasiasa wa kweli, achilia mbali mpinzani.Hata ndani ya CCM alimokuwa, Alikuwa na matamshi yaliyosheheni utata,turudisha kumbukumbu nyima tutamjua Shibuda halisi.