He! Mimi nilikua silijui hili!,
Nimekutana na Mzee mmoja mkongwe wa CCM leo asubuhi mtaani kwetu akanambia; "Aisee CCM wanakiua chama hivi hivi,wanafikiri wamemaliza makundi lakini subiri utajionea mwenyewe!Eti huyu ndio aje kua M/kiti wa chama! yaani wao badala ya kuchagua kiongozi mwenye historia ya kukiongoza chama na kukijua vizuri, leo wamekosa kiongozi mwenye sifa mpaka wakachagua mtu ambaye hata hajui CCM imeanzia wapi?
Yeye anajua tu idadi ya barabara na samaki tu! Haujui hata muundo wa uongozi wa ndani ya Chama, Ni bora hata ya Mwigulu ambaye ndani ya muda mfupi nafasi ya N/katibu mkuu CCM bara kakifahamu chama vizuri, ni bora hata Lowassa pamoja na kuhama kwake lakini anajua namna vyama vinavyoendeshwa kwa uzoefu wake wa uongozi wa miaka mingi ndani ya CCM"
Aidha huyo mzee akaendelea kusema kwamba" Angalia hata kampeni za Magufuli! ni za hofu,jazba,kutetemeka, kukosa kujiamini mbele ya umma, Lakini Lowassa yeye hana hofu anafanya yake kimya kimya akijiamini kua Magufuli sio size yake! kwahiyo kijana ukweli tunaujua asikudanganye mtu"