leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,583
- 3,181
Jamii Forum ni mtandao wa kijamii kama ilivyo mitandao mingine ya kijamii duniani ambapo matumizi makubwa ya mitandao hii imekuwa ni kupashana habari na majukwaa ya kubadilishana taarifa, ujuzi, utamaduni na vitu vingine mbalimbali.
Mitandao hii imegeuka kuwa mwiba mkubwa kwa wanasiasa hasa wa Kiafrika,na sababu kubwa ikiwa ni kuwa kwa muda mrefu wamekua wakivibana vyombo vya habari rasmi, kwa kutumia sheria kandamizi na kuvifanya vishindwe kukidhi kiu ya walaji wa habari, na kwa kutumikia mabwana wawili yaani wanasiasa na jamii ambayo kwa muda mrefu ikivituhumu vyombo vya habari aidha kuficha ukweli kwa kisingizio cha kulinda amani na utulivu.
Ujio wa mitandao ya kijamii uligeuza kila mtu kuwa mwanahabari huru, hivyo udhibiti wa nini kisemwe lini,wapi kwa namna gani ukatoweka ghafla na wahanga wakubwa wa hali hii wakawa wanasiasa.
Nini kifanyike ili wawe salama.
kwani kunashindikana nini kwa watuhumiwa kumwanga hesabu mezani ili kumaliza ubishi.?
Kwa maoni yangu sheria kandamizi, vitisho,kukamata au kufikiria kufungia mitandao havisaidii zimwi ameshatoka kwenye chupa, cha msingi tabia zibadilike mtasifiwa sana humuhum mitandaoni.
Kwa leo ni hayo tu waheshimiwa.

- Lazima wakubaliane na hali halisi usukani ulisha pokonywa si rahisi kuurejesha
- Wanapaswa kuwa wakweli kuliko wakati mwingine wowote teknolojia imebadilika wao hawajabadirika bado wanadanganya asubuhi mchana wameshaumbuka