Wasichana/Wanawake waliowahi kuwatongoza wanaume njooni mshuhudie

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Habari wakuu,


Enzi za wazazi wetu ilikuwa ngumu sana kwa msichana kumwambia mwanaume nakupenda.

Ila siku hizi kwa msichana kumwambia mwanaume nakupenda imekuwa ni kawaida.

Na hii imesababishwa na utandawazi, lakini imesaidi wasichana nao kueleza hisia zao kwa wanaume wawapendao.

Tuje kwa yaliyowahi nikuta;

Nimeamua kuandika haya kwakuwa yalinikutaga kabla sijampata baba watoto wangu..ilikuwa hivi;

Nilitokea kumpenda kaka mmoja tena alikuwa na umri kunizidi, nikawa najaribu kuwa karibu nae nikihisi kuwa angekuja kuniambia ananipenda ajabu ni kuwa haikuwa hivyo, siku zikaenda.

Siku moja tukiwa hoteli fulani nilimuona, nilimfuata na tukawa tunaongea namna ya kufanya (marketing) basi nikapata chance tukabadilishana namba na ndio ikawa mwanzo wamawasiliano, mwishowe tukawa tunatoka naye.

Nakumbuka siku hiyo tukiwa katika gari nilishindwa kujizuia nikajikuta nishamwambia nampenda, alinikiss na mapenzi yakaanza..nilichukia kutongoza ila ndio hivyo ''penzi ni kikohozi ukilificha huliwezi''.

Nifupishe tu...Mwishowe niliona hanipendi na alikuwa haonyeshi kujali hisia zangu..niliumia sanaa..nililia na kujuta kumwambia nampenda.. kwakuwa ilikuwa ngumu kumtoa moyoni ila nikaamua kumuacha kwa shida sana.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom