Washairi nijibuni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washairi nijibuni.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mpemba mbishi, Feb 12, 2012.

 1. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwerekwekwe msumeno.....Kukata ni
  kazi yake
  Kibogoyo aso meno.....Muhogo adhabu
  kwake
  Malenga nna kineno.....Nipeni upeo
  wake KILA TAWI NSHIKALO.....MWENZENU
  LANITELEZA Nilikua kileleni.....Tayari nimetulia
  Najipanga kwa makini.....Matunda
  kujichumia
  Sijui kama ni jini.....Lililo nielemea
  KILA TAWI NSHIKALO.....MWENZENU
  LANITELEZA Purukuchu taratibu.....Chini nilianza
  kuja
  Sikuijua sababu.....Ya kuja moja kwa
  moja
  Katika kupata tabu.....Nikashika tawi
  moja KILA TAWI NSHIKALO.....MWENZENU
  LANITELEZA Cha ajabu likayumba.....Nalo likaniteleza
  Nikamuomba Muumba.....Nipate pa
  kushikiza
  Mungu si bwana Mkubwa.....Hafula
  likatokeza
  KILA TAWI NSHIKALO.....MWENZENU LANITELEZA Nikashukuru Manani.....Nikiona kama
  ndoto
  Hafula mara mwilini.....Nahisi kwawaka
  moto
  Kutizama kwa makini.....Kumbe lina
  majimoto KILA TAWI NSHIKALO.....MWENZENU
  LANITELEZA Tawi lililofuatia.....Halikua na uhaba
  Kwani nililivamia......Likanichosha kwa
  miba
  Si haba nimeumia.....Jama musinite zoba
  KILA TAWI NSHIKALO.....MWENZENU
  LANITELEZA Mti huu siujui.....Mwenzenu bado mgeni
  Una wingi wa matawi......Unapendeza
  kwa nyani
  Nipo chini sijijui.....Najiuguza mwilini
  KILA TAWI NSHIKALO......MWENZENU
  LANITELEZA Nipeni ufafanuzi.....Mti huu mti gani
  Pengine nyinyi wajuzi.....Hamutoka
  maporini
  Nimepona hivi juzi.....Na mti siutamani
  KILA TAWI NSHIKALO.......MWENZENU
  LANITELEZA.
   
Loading...