Wasanii na mavazi mnaikera jamii

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,810
2,0001)Mnawaiga wazungu,kuvaa vaa vinguo
Mwaonyesha ya uvungu,mili inamichubuo
Kwanza mwanuka ukungu,hajajifanya kaguo
Wasanii na vinguo,mwaaibisha taifa.


2)Vinguo vyenu vifupi,si ujanja ni ushamba
Sanaa yenu ni ipi,kuonyesha lambalamba ?
elimu yenu ni ipi,kwa ushamba mnatamba
Wasanii na vinguo,hivi mnauza nini ?


3)Wengine ni nusu uchi,hao ndo malimbukeni
Wanajiona wabichi, wamekomaa usoni
Ni washamba wa kijichi,wameingia mjini
Wasanii na vinguo,badilisheni tabia.


4)Mnengevaa nguo ndefu,si mngelionekana
Mnakuwa kama wafu,natamani watukana
Kwa ujinga mwajisifu,kumbe mnadanganyana
Wasanii na vinguo,mnaufanya utoto


5)Eti tuuze ulaya,ndivyo mnavyofikiri
Nguo hizo za malaya,acha niwape habari
Tena ni tabia mbaya,pia acheni kiburi
Wasanii na vinguo,Tumezidi kuwachoka


6)Tunawahisi wazazi,wenu hawajawafunza
Acheni tuseme wazi,ili muweze jitunza
Mnafanya upuuzi,kama mnang'atwa funza
Wasanii na vinguo,mnajishusha thamani.


SHAIRI -WASANII NA VINGUO
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255626010160
iddyallyninga@gmail.com
 

mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
5,112
2,000
Idd Ninga umekosea kidogo, hawa wasanii wetu uchwara wanaiga wamarekani weusi kwa kiasi kikubwa tu. Utakuta mtu kakulia Tandale, leo hii anajifanya bonge la mshua kwa kuongea kiingereza ambacho hata yeye mwenyewe hajuwi anaongea nini. Mara avae hereni, sijuwi atoboe pua kujifanya shoga, ashushe suruali mpaka mkun.duni, na kujichora mwili kuwaiga wamarekani weusi wakati kiuhalisia mmarekani mweusi hana thamani kwa mwafrika, yaani they don't give a damn kuhusu mwafrika ila sie huku tunaona ujiko kuwaiga na kujifananisha nao, why? Wanawake wetu wasanii ndo kabisa, yaani useless to the point of no return, hawajitambui hata kidogo. Serikali ispofanya jitihada za kuua bongo fleva tutapoteza kizazi cha kesho kwani vijana wako too useless kuiga maisha ya wasanii wa bongo fleva ambayo nayo wasanii wa bongo fleva wanaiga toka Marekani bila hata kujuwa uhalisia wake kwa taifa letu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom