Wasambazaji wa sukari wafutwe

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Tumeshuhudia kuwa wasambazaji wa sukari ni maadui wa wananchi kwa kuficha bidhaa hii wakati wa uhaba, napendekeza wafutiwe uwakala na badala yake viwanda viweke bohari kila Mkoa na wauzaji wote wa jumla wanunue sukari hapo badala ya watu wachache kuwa middlemen wa kuwatesa wananchi.
 
Hilo wazo lako umelifikiria wewe na nani?kwa hiyo hutaki tufanye Biashara?usiwalaum wauza sukari bali tuna shida ya mfumo
 
Tumeshuhudia kuwa wasambazaji wa sukari ni maadui wa wananchi kwa kuficha bidhaa hii wakati wa uhaba, napendekeza wafutiwe uwakala na badala yake viwanda viweke bohari kila Mkoa na wauzaji wote wa jumla wanunue sukari hapo badala ya watu wachache kuwa middlemen wa kuwatesa wananchi.
swala ni yule msitaafu aliyekwenda ikulu na kumwambie mkuu kuwa yuko na mashamba ya miwa mtibwa na kwingineko kwa hiyo stopisha kuleta sukari ili niuze hii miwa hapa ndani kwa bei ya kujipangia.

swissme
 
Tumeshuhudia kuwa wasambazaji wa sukari ni maadui wa wananchi kwa kuficha bidhaa hii wakati wa uhaba, napendekeza wafutiwe uwakala na badala yake viwanda viweke bohari kila Mkoa na wauzaji wote wa jumla wanunue sukari hapo badala ya watu wachache kuwa middlemen wa kuwatesa wananchi.

matatizo mengine ni ya kujitakia tu, sukari hatakiwi kuadimika maana ipo na inatengenezwa hapa nchini na nje ya nchi. Kwa nn mafuta ya kupaka hayaadimiki bali iadimike sukari tu? Kwanini nyama ya kuku haiadimiki bali inaadimika sukari tu? Serikali kama imeshagundua ilifanya haraka sana kuzuia uagizwaji na usambazaji wa sukari basi wafanye u-turn kwa haraka. Kama issue utaratibu haukuwa mzuri ni kuubadilisha tu kwa uharaka na kuhakikisha sukari inakuwepo ya kutosha.
 
Kuna watu wanatumia makalio kufikiria! Eti viwanda vijenge bohari kila mkoa! Utawajengea wewe? Uchumi huru na biashara huria....demand and supply ndio inatamalaki na kuendesha bei ya bishaa! Serikali inatakiwa kuchukua kodi na control inflation pamoja na kuhakikisha bidhaa ipo kwa wingi kuongeza waagizaji na kuregulate policy na kodi kama ni lazima
 
Back
Top Bottom