Wasaka Urais msirudi tena Majimboni

Wasaka Urais msirudi tena Majimboni

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Mnachogombania mking'ang'anie.Mkikikosa basi.Majimbo hayatawahusu tena. Hamtakuwa na nafasi ya kutaka Urais na Ubunge kwa pamoja. Mkae mkijua kuwa watanzania wanataka kuanza kuiona safu ya Wabunge,Madiwani na Rais wao. Wasaka Urais muwe makini.Mjipange kwelikweli.Mtapaswa kuusaka Urais na uraia,yaani,mkikosa Urais mtakuwa raia wa kawaida.

Hatuna haja y watu wanaotaka kuhodhi kila uongozi. Mwaka huu ni tofauti. Hatutaki makapi yabaki. Mjiandae kisaikolojia!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
wasirudi wakati ccm mmeweka mkakati wa kukata majina unategemea nini mkiwakata
 
Ukitaka kuona wengi wakipoteza maisha kwa shinikizo la damu miongoni mwa wasaka urais ebu pitisheni hiyo hoja muone!!!!
 
MAZITO YAVUJA KIKAO CHA WENYEVITI WA MIKOA CCM,BARUA YA KINANA YAKOSOLEWA.

Katika kikao cha wenyeviti wote wa CCM wa mikoa kilichofanyika katika ofisi ndogo za Lumumba jijijin Dar es Salaam jana tar.24. Wenyeviti hao wakiwa katika kikao chao kilichokuwa kinajadili mambo mbalimbali ya chama na utekelezaji wa mambo ya Uchaguzi, walipofika kwenye agenda ya ujenzi wa chama walionekana kusikitishwa kwao kwa katazo alilopewa Naibu katibu Mkuu wa CCM ndg Nchemba huku akiwa ametokea kufanya kazi nzuri ya uimarishaji wa chama.

Akiwa wakwanza kuchangia hoja hiyo mwenyekiti wa Manyara Ole Muksi alisema "tumeshangazwa sana na Barua ya Katibu Mkuu kwenda kwa Naibu wake, Kwanza Mwigulu alikuja Wilaya zote za Mkoa wangu wa Manyara, Kote alikopita tumeshinda kwa kishindo, tumeshinda mpaka karatu mwenyekiti, tumepata vijiji kwa ushindi mbulu, Hydom, kubwa zaidi Mwigulu hakuongelea mambo ya Urais wala kutaja jina lake wala kusema na mjumbe yeyote.
Kumwandikia barua kwa fitna itavunja moyo watu wanaojitolea kujenga chama. Binafsi sikuona kama sababu ni urais labda sababu ni kukubalika kwake, sasa hili pimeni kama linakijenga chama au tunabomoa chama.
Alipokuaja tulipata watu zaidi ya elfu sita saa tatu asubuhi na zaidi akamng'oa katibu wa CHADEMA wilaya ya Karatu, haijawahi tokea. Chama inabidi itathimini upya katazo hilo. Chama hakiwezi kujengwa na Nape na kinanan pekee yake,Kama shida ni unaibu wamtoe unaibu lakini sio kumzui kazi za unaibu.

Naye Mama Buhiye mweneyekiti wa CCM kagera alisema "Mwigulu alitusaidia sana, tena tunaomba aje tena, kwa kweli hakuonesha wala kuongelea Urais. Pia hakukutana na kiongozi yeyote wa kagera. Tofauti na wengine yeye alikuwa akimaliza mkutano anaruka kumaliza na kuruka na jion hata chakula cha pamoja hakikwepo. Wasimwone kiasi hicho. "
Wakati huo huo Dr Kaburu mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma alisema "CCM isitengeneze chuki na vijana, mpaka sasa uraiani inasemekana kuwa sisi tunamziba mdomo kijana ambaye hajui kupendelea kitu , kisa alisemea kuwa wezi wa escrow wafilisiwe, kisa alisema kodi kwenye escrow irudi ni ya umma. Kisa aliongea kwenye katiba, kisa anakemea uovu wa baadhi ya watendaji wa serikali.Picha hii sio nzuri kwa Chama na watanzania, kumzui kufanya mikutano mtu ambaye amekua bega kwa bega Kuimarisha CCM . Sisi tumemwalika tangu mwezi wa tisa mwaka jana kwa kikao cha kamati ya siasa, nimeambiwa tanga walimwalika tangu mwezi wa kumi, kama ilvyo mara na shinyanga tena kwa barua, waache kugawa chama. Mimi nimempigia Kinana kumlalamikia hili, hata yeye halmjengi. Tunaomba makao makuu iangalie upya katazo hilo. Huyu ni naibu katibu mkuu sio personal assistant."

Hali iliendelea kuwa ya utulivu zaidi baada ya Saanya Mwenyekiti wa Mara aliposema makamanda wake walikataa kuapishwa na mtu mwingine na tulimwalika tangu mwezi wa nane. "Wananchi mara wamerudisha imani kwa Chama hivi majuzi baada ya Mwigulu kuweka mambo sawa pale Msoma,watu waache wivu, Mwigulu hakuongelea mambo ya Urais alikijenga chama.

Msukuma Mwenyekiti wa Geita aliyekuwa kwenye mizunguko na Mwigulu alisema "helkopita isiwe nongwa, Nilimkaribisha Mwigulu, tulishatumiaa helikopita hiyo na Dialo wilaya zote za Mwanza, na Makonda wilaya zote, na Mama Tibaijuka kagera yote, na Lameck Airo jimbo lake lote. Hii isiwe nongwa. Kijana anakubalika, anajenga chama tuache wivu na kusingizia helkopita. Sisi Geita tumeandika barua kumwita.
Dialo alithibitisha kuitumia helkopita hiyo. Ni kweli mwenyekiti nimetumia helkopita hii. Labda tuambiwe kama kwenye chama chetu ni kosa, wala sio kwa Mwigulu tu.

Kwa upande wake Kimbisa alisema jambo hili lilipaswa lipitie vikao kabla ya barua, sisi Kamati kuu hatujawahi kujadili jambo hilo. Baraua imeandikiwa Zanzibar hivyo nadhani utaratibu wa CCM hata kwa mpika chai uamuzi hufanyika kwa kupitia vikao. Nasubiri taarifa ije kamati kuu"
Wakati hayo yakiendelea,Baadhi ya wenyeviti walikuwa na sauti za chini kuwa CCM haijengwi na watu wawili tu,Chama kinajengwa na wanachama na Viongozi wote.

My take, Chama Cha Mapinduzi ni kikongwe na kinajua namna ya kudeal na Mambo madogomadogo kama haya,Urais kwa mwenendo huu utapelekea wananchama na Viongozi wasifanye kazi ya chama,CCM ni Zaidi ya Urais.
 
tatizo la ccm kila kada anaona anaweza kuwa rais ndo maana wengi wanatangaza nia
 
My take, Chama Cha Mapinduzi ni kikongwe na kinajua namna ya kudeal na Mambo madogomadogo kama haya,Urais kwa mwenendo huu utapelekea wananchama na Viongozi wasifanye kazi ya chama,CCM ni Zaidi ya Urais.​
Mwigulu savimbi Investment T Ltd.
dealing with kujipigia machapuo, ugaidi, kupiga proganda mfu.
TUPO LUMUMBA NA DODOMA
 
Back
Top Bottom