Lipangwalo na Mungu halipanguki. Kuna siku bus lilikua linatoka Dar kuelekea mkoani. kutokana na uchovu wa safari,karibu abiria wote walikua usingizini. Wakati dereva akiendelea kuendesha bus, ghafla kuna lorry lilijitokeza hivyo dereva wa bus ikabidi atumie akili ya ziada kulikwepa lile lorry. Wakati huo siti ya pembeni mwa kiti cha dereva kulikua kuna mdada alikua macho akishuhudia tukio hilo linavyokuja hivyo aliamua kujirusha kupitia dirishani kwa kuhofia kufa ambapo ktk kutua ardhini,abiria yule alibamiza kichwa kwenye jiwe kubwa na kufariki papo hapo. Ktk jitihada za kulikwepa lorry lile,bus lilipinduka na hakuna yeyote aliyefariki zaidi ya yule abiria aliyejirusha mwenyewe dirishani. Hapa inaonesha kwamba kama imeandikwa siku flani utakufa,basi huna ujanja wa kukwepa usife