SILENT GUNNER
Member
- Jan 23, 2012
- 22
- 9
Jamani kama mwanachama wa chadema na mwenye mapenzi mema na chadema,nimemsikiliza shibuda akihojiwa na radio one katika kipindi cha nipashe asubuhi na nimeamini kweli ana kusudia kugombea urais,pamona na lengo lake nimemsikia akiwa na mtazamo wa kukikandia chama et ni cha kidictator na ukabila. jamani hamna namna ya kuliengua hili gamba? najisikia hasira nikikumbuka uwepo wa jitu kama hili chadema. Anawezaje kulala chadema kula ccm? na kwann aombe msaada jk amsaidie kama sio jitu lililotumwa na magamba? Lets he careful kupokea mtu na kumpa madaraka
Nakubaliana na wewe kuwa hata akifukuzwa uanachama, bado ataendelea na ubunge kwa amri ya mahakama pengine hadi uchaguzi mwingine 2015. Kuna haja ya kuangalia sheria hii. Hivi ikija kuthibitika mahakamani kuwa Kafulila au Hamad walifukuzwa uanachama kihalali, hii mishahara na posho wanazoendelea kulipwa watazirudisha hazina? Wanasheria tusaidieni katika hili.Chadema needs high technicalities to get rid of this stupid guy!! wasikurupuke, atakwenda mahakamani atawashinda kama hawajamwekea mtego wa kisheria/kichama wa/kikatiba ya CDM kumnasa na kumtema. Si vizuri jitu kama hili kwenda mahakamani likakushinda!!! Historia hufunza , si tunaona akina Hamad Rashid et al wote wako mahakamani, wakifanya ubunge wa mahakama!!!
Bwana Komandoo na wengine msiwe na wwasi wasi na hkuna sababu ya kumpiga chini bw Shibuda. CHADEMA ni chama makini na kila mtu ndani ya chama ana uhuru wake ila chama kina taratibu zake. Hata watoto wa familia moja hawafanani lakini wote ni watoto wa alio nao.Huyu ni wa kupiga Pichi ili aungane na wakina Kafurila, Rashidi Mohamed katika Ubunge wa Mahakama, najua akipigwa chini atachonga sana, ila ni wa kupiga chini tu, na CHADEMA wahakikishe 2015 hakanyagi Bungeni kwamwe ni Bora kilikosa Jimbo kabisa lakini asikanyage Bungeni kwa Tiketi ya Chama chochote kile, Ndo dawa yake,
CDM ndio wanatakiwa kujifunza. Huyu alipopigwa chini kura za maoni, alisema wazi kuwa anatafakari aende wapi, lakini pia akasema kuna vyama zaidi ya vitatu vimemuomba ajiunge navyo. Pengine kwa kiu ya kuongeza viti au kuogopa kuwahiwa na vyama vingine, CDM kupitia kwa Zitto (Atanisamehe kama sivyo) ndio waliokwenda kumuomba ajiunge nao....
Huyu ni zaidi ya Kinyonga, nakumbuka wakati alipigwa chini CCM kwenye kura za maoni aliichuria CCM ile mbaya, na shangaa juzi kuanza kuwasifia, na hata huko CCM KUNA ANACHO TAFUTA,