Warioba, Butiku na Pole Pole kuisifia Katiba pendekezi ya Sitta ni kula matapishi yao au ni usaliti?

gps boy

JF-Expert Member
Oct 3, 2015
447
65
Hakika nchi hii viongozi wa kushangaza sana. Mwenyekiti wa tume ya Katiba na baadhi ya wajumbe wake Mzee Butiku na Bw.Polepole wakati bunge la katiba lilipoiponda rasimu yao walihaha nchi nzima kuhamasisha Wananchi wasiipigiekura katiba Pendekezi ya Mzee Sitta na kuandaa midahalo Nchi nzima kupinga.

Midahalo iliyopelekea Mzee warioba kutukana matusi ya nguoni na wajumbe na wabunge wa CCM wenzake na mwisho kutandikwa makofi na Kijana mtovu wa adabu makonda na kisha kupongezwa na kupewa ukuu wa wilaya.

Cha kushangaza Mzee Warioba na hao wajumbe leo Wameigeuka Rasimu yao wanaisifia katiba pendekezi ya Mzee Sitta.Tunajiuliza wameamua kula MATAPISHI au kuwasiliti ,wananchi au ndio njaa kali.
 
Wewe ni muongo ....umesikia wapi wakisifia Katiba ya Sitta iliyoandaliwa na akina Chenge rafiki mkuu wa "bwana mkubwa" .....waliozima katiba ya Warioba wamekwenda Chadema ....akiwemo Kingunge aliyesema ajenda ya Katiba si ya CCM bali Kikwete ....zindukeni ache ushabiki tu ....
 
hajasifia unapotosha mkuu.

ila anachokifanya warioba na wenzake ni kukulazimisha CCM irudi madarakani ili ipitishe KATIBA ILIYOANDIKWA NA WAKINACHENGE.

HApo ndipo utajua watanzania ikifika siasa siop mzee,kijana karibuwote huwa tunajipofusha na kuwa watu wa ovyo. Ila hii imekithilikwa wenzetu wa chama tawala.
 
hii inakuwa ni njaa tu na tamaa,ndio system ya tz ilivyowaweka watu wake kuwa tegemezi kwenye system,ili kila mtu awe kama karagosi,hakuna thamani utu
 
hii inakuwa ni njaa tu na tamaa,ndio system ya tz ilivyowaweka watu wake kuwa tegemezi kwenye system,ili kila mtu awe kama karagosi,hakuna thamani utu

Asante Mkuu! THAMANI UTU neno muhimu sana linatakiwa kuzingatiwa na wananchi.
 
Acha wayale mbona mbowe, lissu, mnyika, lema na msigwa ameshakula matapishi yao kuhusu lowasa.
 
Back
Top Bottom