Warioba anafanya kazi hii kwa niaba ya nani? Huo ni uchochezi

chawade

Member
Nov 21, 2014
21
3
CHAMA CHA WANANCHI NA DEMOKRASIA (CHAWADE)
S. L. P 90041- DAR ES SALAM
Tel 0789 113534.
10/11/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WARIOBA ANAFANYA KAZI HII KWA NIABA YA NANI? HUO NI UCHOCHEZI.

Sheria ya mabadiliko ya Katiba sura 83 toleo la mwaka 2014 toleo liliorekebishwa la mwaka 2014 ninazingatia na kuwekwa pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika sheria hii ilipotungwa mwaka 2011 hadi tarehe 31 Disemba 2013 na likachapishwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha sheria ya urekebu sheria, sura ya 4.

Sheria ya mabadiliko ya katiba ilitolewa Disemba mosi 2011 kwa ajili ya kuunda Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa madhumuni ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba, kuainisha na kuchambua maoni ya wananchi, kuianisha masharti kuhusu mabaraza ya kutoa uamuzi juu ya rasimu ya katiba, kuweka masharti juu ya utayarishaji na uwasilishaji wa ripoti kuhusu maoni ya wananchi, kuweka utaratibu wa kuunda Bunge maalum, uendeshaji wa kura ya maoni na kuweka masharti yanayohusiana na mambo hayo. Sheria Na 8. ya mwaka 2011, Na 2. ya mwaka 2012, Na 7. ya mwaka 2013 Na.9 ya mwaka 2013, Na 11 la mwaka 2013 na tangazo la Serikali Na. 394 na mwaka 2011.

Aidha Katiba hii iliyopendekezwa imetokana na mjadala wa Bunge maalum la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilioundwa chini ya kifungu cha 22 .

Baada ya kutunga Katiba iliyopendekezwa, masharti yatokanayo na masharti ya mpito, Bunge maalum litavunjwa na mamlaka ya kutunga masharti yatokanayo na masharti ya mpito yatakoma na (Sheria Na 7 ya mwaka 2013 kifungu cha 10 Tangazo la serikali Na. 394 la mwaka 2011 amri ya 2 aya (u).

Baada ya kuwasilishwa kwa rasimu ya Katiba kwenye Bunge maalum chini ya kifungu cha 20 (3) Rais kwa amri iliyochapishwa kwenye gazeti la Serikali , ataivunja Tume. Kuvunjwa kwa Tume kwa amri ya Rais kutakuwa na maana ya ukomo wa mamlaka ya Tume na Sekretarieti.

Sheria imeainisha matukio hatua ipi itafanya nini na wakati gani, Tume ya Warioba ilimaliza muda wake na kazi zake pale alipokabidhi rasimu ya pili ya Katiba kwa Rais ili rasimu hiyo ikajadiriwe na Bunge maalum la katiba. Nalo Bunge maalum la Katiba lilimaliza kazi yake pale Katiba ilivyopendekezwa ilipowasilishwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kwa Rais.

Aidha Sheria inaidhinisha kuwa hatua inayofuata sasa ni kuipeleka Katiba inayopendekezwa kwa wananchi na hatimaye kupigiwa kura ya “ndiyo” au “hapana”. Je Warioba na wajumbe wake wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba wanapofanya midahalo kuonyesha misimamo yao, na kudai ndiyo misimamo ya wananchi wanatoa picha gani? Si wawaachie wananchi wakaamue wenyewe kwenye kura ya maoni? Wanandhi ndo waseme haya yaliypendekezwa na Bunge maalum siyo maoni yetu na wala sio warioba na kundi lake. Hii inatoa picha kuwa hata yaliyokuwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba ni maoni yake (Warioba) na wenzake na wala si ya wananchi. Kama ni maoni ya wananchi waache wakaseme kuwa sio maoni yao. Warioba asinyakue mamlaka ya wananchi na kujifanya anatetea wananchi kama walivyojinyakulia UKAWA. UKAWA wanadai Katiba ya wananchi, wananchi hawajawatuma, lakini wao wanadai wanawakilisha; Je! Wananchi wanawatazamaje? Leo ukiwa msaliti kwenye kundi lako unaitwa UKAWA mfano Simba UKAWA n.k.

CHAWADE kinazidi kutokubaliana na Jaji warioba kuendelea kuijadili Katiba iliyopendekezwa kwani huu si wakati wake, huku ni kuwachochea wananchi wafanye maamuzi yasiyojitegemea badala yake wafuate mawazo ya Warioba na ama taasisi ya mwalimu Nyerere au kikundi kidogo cha watu wenye chuki binafsi na Serikali huku wakitumia mgongo wa kile kinachoitwa wananchi.

Mchakato wa Katiba ni jambo la kisiasa lenye kutafuta muafaka na maridhiano lakini pia ni kukubali nguvu ya umma (yaani wengi) Katika maamuzi; Bunge la katiba lilikuwa na jukumu la kutunga katiba na lisingelazimishwa kutumia muundo wa maneno ya Tume ya warioba na wala Tume ya Warioba haikupewa kazi ya kutunga Katiba bali kukusanya maoni ya wananchi, kuainisha na kuyachambua na kuandaa rasimu ya kwanza na ya pili. Aidha mchakato umeonyesha wazi ni wapi Tume ya Warioba ya mabadiliko ya Katiba inapoishia. Anayofanya Warioba sasa hivi ni kutumia Sheria Na ngapi ya mabadiliko ya Katiba? Namba 8,2,7,9 au 11? Warioba na kundi lake waache kuwachochea wananchi kwa dhihaka ya kuwasemea. Nani kawatuma katika hata hili? Eti tutakutana mtaani!!! Mkutane mtaani ili mfanyeje? Kilichompata Ubungo Plaza kwenye hotel ya Blue Peal wakati akiwasilisha mada, mdahalo ulioandaliwa na Mwalimu Nyerere Fondation ndio hasa alichokifuata mtaani kwani hayo ndo mambo ya mtaani kama anayatafuta. Warioba auache mchakato ulipofikia kwa wenyewe (wananchi) waamue muda ukifika.

Imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi na Demokrasia (CHAWADE) Makao Makuu November 2014
(CHAWADE KWA POMOJA TUTASHINDA)Shabir Mpaka
Mwenyekiti – Taifa.
 
Kweli wewe Na kundi lako Ni CHAWA, mnang'ata nguoni. Warioba yeye siyo Mwananchi? Kwani akiongea Na kutoa maoni yake shida iko wapi? Watamsikiliza and if he makes no point atapuuzwa. Wewe tulia wananchi ndo wataamua wenyewe.
 
Nguruwe utawajua Tu hawajui kipi ni chakula na yapi ni maji maana nguruwe hula Hata kokoto jueni kubakiza maneno
 
Naona mtoa mada ametumwa kupima upepo. Ngoja escrow iishe halafu utukumbushe tena juu ya hili
 
maandishi meeengi utafikiri ni wananfunzi wa sekondari east afrika wanaoshindanishwa kuandika ESE.
 
Waryoba aliishaeleza kwamba anatoa mawazo haya kama raia. Kosa liko wapi? Mbona inakuwa nongwa mtu akijitokeza kueleza mapungufu ya Katiba Pendekezwa lakini inakuwa sawa mtu akisema inafaa? Nini kinachowahofisha? Na wewE CHAWADE umeibukia kutoka wapi? ndo kwanza nakusikia leo. Nahisi unajiwakilisha mwenyewe!
 
Kama raia kwani yeye ni Raia first class sisi wengine third class
 
Chawade ni nini? Ni NGO au Chama cha Siasa! Kwenye BMK waliwakilishwa au walipeleka mapendekezo yao kwa Sitta kama wale wengine!
 
ukiambiwa nawe changanya na zako, we unatumwa kuleta upuuz hata hukuhoji kuwa jamii forum kuna wasomi? unaleta upuuz wako ukitegemea kunamtu wa kuacha vitu vya msingi na kujadili upuuz? nahisi ungepeleka kwa waliokutuma wambie labda waandae mbinu nyingine. hiyo ni ya kizamani mno. shame on you
 
Hakuna mtoto wa chekechea humu ndani wa kumuongopea kama umetumwa kajipangeni upya...
 
chawade ili ifanane na cdm, ujinga mwingine bwana,unataka kupata kiki kuwa umekuja na habari mpya,wewe ni wa kupuuzwa,kazi anayofanya mzee waryioba inatakiwa kuungwa mkono nawatz wote utaenda kupiga kura bila elimu ya kutosha kuhusu hiyo katiba, muda uliowekwa hautoshi na watoaji elimu hawaeleweki,hivyo unaposema kuwa ni uchochezi unamaana gani anamchochea nani dhidi ya nani,maisha ni magumu sana kamaunataka huruma ya watawala kwa kuonekana unaoupande mmoja tafuta namna nyingine hii hata wao wanajua huwasaidii,mwacheni waryioba awaelimishe watanzania mazingaombwe yenu yajulikane kwa uwazi.
 
CHAMA CHA WANANCHI NA DEMOKRASIA (CHAWADE)
S. L. P 90041- DAR ES SALAM
Tel 0789 113534.
10/11/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WARIOBA ANAFANYA KAZI HII KWA NIABA YA NANI? HUO NI UCHOCHEZI.

Sheria ya mabadiliko ya Katiba sura 83 toleo la mwaka 2014 toleo liliorekebishwa la mwaka 2014 ninazingatia na kuwekwa pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika sheria hii ilipotungwa mwaka 2011 hadi tarehe 31 Disemba 2013 na likachapishwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha sheria ya urekebu sheria, sura ya 4.

Sheria ya mabadiliko ya katiba ilitolewa Disemba mosi 2011 kwa ajili ya kuunda Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa madhumuni ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba, kuainisha na kuchambua maoni ya wananchi, kuianisha masharti kuhusu mabaraza ya kutoa uamuzi juu ya rasimu ya katiba, kuweka masharti juu ya utayarishaji na uwasilishaji wa ripoti kuhusu maoni ya wananchi, kuweka utaratibu wa kuunda Bunge maalum, uendeshaji wa kura ya maoni na kuweka masharti yanayohusiana na mambo hayo. Sheria Na 8. ya mwaka 2011, Na 2. ya mwaka 2012, Na 7. ya mwaka 2013 Na.9 ya mwaka 2013, Na 11 la mwaka 2013 na tangazo la Serikali Na. 394 na mwaka 2011.

Aidha Katiba hii iliyopendekezwa imetokana na mjadala wa Bunge maalum la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilioundwa chini ya kifungu cha 22 .

Baada ya kutunga Katiba iliyopendekezwa, masharti yatokanayo na masharti ya mpito, Bunge maalum litavunjwa na mamlaka ya kutunga masharti yatokanayo na masharti ya mpito yatakoma na (Sheria Na 7 ya mwaka 2013 kifungu cha 10 Tangazo la serikali Na. 394 la mwaka 2011 amri ya 2 aya (u).

Baada ya kuwasilishwa kwa rasimu ya Katiba kwenye Bunge maalum chini ya kifungu cha 20 (3) Rais kwa amri iliyochapishwa kwenye gazeti la Serikali , ataivunja Tume. Kuvunjwa kwa Tume kwa amri ya Rais kutakuwa na maana ya ukomo wa mamlaka ya Tume na Sekretarieti.

Sheria imeainisha matukio hatua ipi itafanya nini na wakati gani, Tume ya Warioba ilimaliza muda wake na kazi zake pale alipokabidhi rasimu ya pili ya Katiba kwa Rais ili rasimu hiyo ikajadiriwe na Bunge maalum la katiba. Nalo Bunge maalum la Katiba lilimaliza kazi yake pale Katiba ilivyopendekezwa ilipowasilishwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kwa Rais.

Aidha Sheria inaidhinisha kuwa hatua inayofuata sasa ni kuipeleka Katiba inayopendekezwa kwa wananchi na hatimaye kupigiwa kura ya “ndiyo” au “hapana”. Je Warioba na wajumbe wake wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba wanapofanya midahalo kuonyesha misimamo yao, na kudai ndiyo misimamo ya wananchi wanatoa picha gani? Si wawaachie wananchi wakaamue wenyewe kwenye kura ya maoni? Wanandhi ndo waseme haya yaliypendekezwa na Bunge maalum siyo maoni yetu na wala sio warioba na kundi lake. Hii inatoa picha kuwa hata yaliyokuwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba ni maoni yake (Warioba) na wenzake na wala si ya wananchi. Kama ni maoni ya wananchi waache wakaseme kuwa sio maoni yao. Warioba asinyakue mamlaka ya wananchi na kujifanya anatetea wananchi kama walivyojinyakulia UKAWA. UKAWA wanadai Katiba ya wananchi, wananchi hawajawatuma, lakini wao wanadai wanawakilisha; Je! Wananchi wanawatazamaje? Leo ukiwa msaliti kwenye kundi lako unaitwa UKAWA mfano Simba UKAWA n.k.

CHAWADE kinazidi kutokubaliana na Jaji warioba kuendelea kuijadili Katiba iliyopendekezwa kwani huu si wakati wake, huku ni kuwachochea wananchi wafanye maamuzi yasiyojitegemea badala yake wafuate mawazo ya Warioba na ama taasisi ya mwalimu Nyerere au kikundi kidogo cha watu wenye chuki binafsi na Serikali huku wakitumia mgongo wa kile kinachoitwa wananchi.

Mchakato wa Katiba ni jambo la kisiasa lenye kutafuta muafaka na maridhiano lakini pia ni kukubali nguvu ya umma (yaani wengi) Katika maamuzi; Bunge la katiba lilikuwa na jukumu la kutunga katiba na lisingelazimishwa kutumia muundo wa maneno ya Tume ya warioba na wala Tume ya Warioba haikupewa kazi ya kutunga Katiba bali kukusanya maoni ya wananchi, kuainisha na kuyachambua na kuandaa rasimu ya kwanza na ya pili. Aidha mchakato umeonyesha wazi ni wapi Tume ya Warioba ya mabadiliko ya Katiba inapoishia. Anayofanya Warioba sasa hivi ni kutumia Sheria Na ngapi ya mabadiliko ya Katiba? Namba 8,2,7,9 au 11? Warioba na kundi lake waache kuwachochea wananchi kwa dhihaka ya kuwasemea. Nani kawatuma katika hata hili? Eti tutakutana mtaani!!! Mkutane mtaani ili mfanyeje? Kilichompata Ubungo Plaza kwenye hotel ya Blue Peal wakati akiwasilisha mada, mdahalo ulioandaliwa na Mwalimu Nyerere Fondation ndio hasa alichokifuata mtaani kwani hayo ndo mambo ya mtaani kama anayatafuta. Warioba auache mchakato ulipofikia kwa wenyewe (wananchi) waamue muda ukifika.

Imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi na Demokrasia (CHAWADE) Makao Makuu November 2014
(CHAWADE KWA POMOJA TUTASHINDA)Shabir Mpaka
Mwenyekiti – TaifaKwanza CHAWADE ni nini? na mnajishughulisha na nini? Swali langu ni je Walioba kawazuia wananchi kupiga kura? Kama maoni ya Walioba si ya wananchi watasema wenyewe na hata wewe si msemaji wa wananchi.
 
Back
Top Bottom