Waridi la moyo wangu

Royal Warrior

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
1,166
Reaction score
2,144
Waridi la moyo wangu,
Tabasamu lako ndio furaha yangu,
Kukupenda ndio chaguo langu,
Muda wote upo kichwani mwangu,

Asubuhi, mchana na jioni,
Sina raha kama sijakutia machoni,
Na usiku nakuota ndotoni,
Kila sekunde upo mwangu moyoni,

Wewe ndio maumivu yangu,
Na wewe ndio ahueni yangu,
Wewe ndio kilio changu,
Na wewe ndio kicheko changu.

....................................................
 
Bila kumtag huyo ua waridi wako ni kazi bure. Au umemwambia PM aje aangalie kisirisiri? Na si ajabu umewaambia hata wawili+ kwa mpigo na sasa huko waliko kila mmoja kavimba kichwa eti ua waridi; na kazi yako iliyobaki ni kuchakata tu. Pyua baharia [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2221][emoji2221][emoji2221]
 
Naona upo na kiswaswadu ufukweni hongera
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na hizo lines zimekaa ki wack, mpe hizi kisha mtag halafu thank me later

Usinipige teke dia, usisepe na usithubutu kuniachia.../

Mtaani kuna vicheche kama mia, hawajatulia wakiona vyepe wanalilia.../

Ila ntatafuta hela ntakugharamia, ntakupa pamba kali hadi shela utafanya la kushindia.../

Nakupenda sana mpaka nimekua mkosefu, siku hizi naona wivu hata ukimpa sifa bwana yesu.../
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania
 
Yametaradadi
Naona kila mmoja anajimwaya mwaya!
Nami ntakuandikia wewe kwa niaba ya wanawake wengine 😉

Waridi la moyo wangu,kulala naona tabu!
Tabibu wa roho yangu,karibu kifuani kwangu..

Moyo uutoe masweke,usiku tuusweke
Nawe punguza mapepe,kitandani uburudike😉

Mwenye utamu uliokithiri,ukinipa sifikiri!
We ni mtamu sio siri,wangu ubani umeusitiri!

Sijui ntakuja kuiona pepo Mimi maana..
 
Awwwwwwwwwww[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8]
Natamani nisiwe naota mimi jamani!!
 
It's Scars.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…