Waraka wa wazi kwa Waziri wa ajira na Rais Magufuli

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,099
8,727
Ndugu wanajamvi,naomba mnipe fursa niisaide serikali ya Mh Raisi, kupitia wizara ya ajira au kazi.

Kwanza nianze kwa kumsalimia Rais, mfanyakazi na muajiriwa wangu, kati ya watumishi wengine wa nchi hii.

Baada ya salam naomba mkuu wa nchi kupitia wizara ya kazi na ajira, niwambie kuwa mimi kijana na wa kitanzania nimekaa chini na kufikiria suluhisho la ajira, suluhusho la waajiri na waajiriwa kukwepa kulipa kodi, suluhisho la wadaiwa wa bodi ya mikopo kutokulipa madeni kwa wakati.

SULUHISHO LA AJIRA.

Mh raisi, unisamehe mimi nimezoea kukuita Braza Magu, ili tuondoe tatizo la ajira lazima kwanza,
tutambue kuwa Tanzania inauitaji wa ajira kiasi gani na kiasi gani kinaitajika kuajiriwa na kwa wakati gani na wapi?

Kwa upande wa fursa za serikalini, wakala wa ajira za serikali anaweza kutusaidia kwa hili kwa kutuambia ni idara gani zinahitaji kuajiri serkalini na kwa wakati gani? Idara zote za serikali lazima zipeleke uhitaji wa watu kwa wakala wa ajira pale, sio ombi ni lazima, hili litasaidia sana kaka Magu, kwanza kusaidia kuondoa rushwa za ajira kwenye taasisi za umma. Bora rushwa ya pesa kuliko rushwa ya NGONO, dada zetu wanamegwa sana Broo Magu.,

Wakala wa ajira ndiye atakuwa na jumla ya ajira zilizotolewa na serikali na kwa kipindi fulani ili linawezekana Broo Magu, mtume wazir wa kazi aseme hivi linawezekana na pia pale utumishi Wazri wa kazi atumbue jipu pale pameoza.

Watu wanafanya kazi kwa mazoea sana nao pia wameleta undugulization sana mahali pale.Wahamishwe waletwe wengine Broo Magu. Hili litaisaidia serikali kujua imetoa fursa ngapi , kwa fursa hizo kodi kiasi gani kimeongezeka na wangapi walisomeshwa na bodi ya mkopo na jewanalipa? i

Pili, Rais Magufuli, mimi nina miezi sta sina kazi, mitandao ya kijamii iliyosaijiwa kwa kipindi hiki ni mingi na yenyewe inafanya kazi nya kutafutia watu kazi. Broo Magu sjui kama inalipa kodi, nitakupa mfano ile moja ilikuwa inaitwa EROLINK, yenyewe ilikuwa inatutaftia kazi alafu inachukua nusu mshahara, mimi ni miongoni mwa watu waliotaftiwa.Nilimuuliza jamaa mmoja pale, sasa mbona mshaara wangu tunagawana sawa? mi nitalipaje kodi ya nchi, na bodi ya mkopo, aliniambia nisiwe na wasiwasi, ataongea na meneja mwajiri wa kampuni nisiwe nalipa kodi wala bodi ya mkopo leo hii eti bodi ya mkopo wananitafta mdaiwa sugu?

Kaka magu ili kuondoa hili, vijizoomtanzania, everjobs, empower, na wengine wote waondoe, kabisa wapige marufuku, alafu nenda pale TEMESA, wakala wa ajira kwa Makampuni binafsi waambie wote kuwa mtu yoyote anaekuja kufungua ofisi Tanzania lazima apitie pale.Hili litatusaidia kwanza serikali kuwa na orodha kamili ya watu wali ajiriwa nchini kupitia private investor na pili, kwa sababu TEMESA ni ofisi yako itakusaidia, kujua wangapi wameajiriwa? ofisi gani? viwango vyao vya elimu, na je walisomeshwa na Bodi ya mkopo au la? je ofisi walizo ajiriwa nazo je zinalipa kodi, na kiasi gani kodi TEMESA imeiingizia serikali kupitia ajira ilizotafta?

Nataka nikwambie kitu kimoja Broo Magu, TEMESA ni jipu kuna vijana pale wanashinda kwenye kazi nyingine hawafanyi kazi zinazotakiwa kufanywa yani wao wanasubiri kuetewa mahitaji ya watu kuajiriwa badala ya wao kutoka kwenda kutafta watu wanaoingia Tanzania kuwekeza na kuingia nao mkataba wa kuwapa vijana wa kazi.

Kaka Magu ili hawa vijana waweze kufanya kazi vizuri lazima kwanza tuwape Target ya watu wanaotakiwa kuajiriwa kwa miezi sita.Haiwezekani watu wanaingia nchini wanatoa ajira serikali haina database inayoonesha watu walio ajiriwa wapi na lini na wanalipa kodi au la wakati wawekezaji hao walipokelewa na moja ya mawaziri wako.

Mimi sikufichi mkuu Broo Magu, asilimia 90 ya wawekezaji wa kichina nchini hawalipi kodi na wala wafanyakazi wao hawalipi bodi ya mkopo mimi nakwambia hili nalijua hata ukitaka nikutajie mfano ntakutajia ila hapa siwezi maana muajiri wangu wa kimagumashi atanisoma na kunifukuza ila kama vipi Broo Magu niinbox twende pamoja.

Waraka huu umfikie Waziri wa kazi na ajira. Lazima nchi kama nchi iwe na database inayoonesha watu wake walio ajiriwa na Serikali na Private instutition. Broo Magu, waajiri wengi wa private nchini ni magumashi ingawa pia kuna watu wameajiriwa serikalini hawalipi kodi hivi hili unalijua Broo magu? Hawalipi bodi ya mkopo Broo walijua hili?

Siwezi sema uongo leo nimeenda kuomba kazi, CANARA Bank. HII ni benki mpya eti wananiambia niende empower wao ndo watanifnyia interview na kunileta na wameniambia kabisa nafasi zipo. Kwenda pale ofisini kwao naambiwa eti nafasi hakuna.Nikahisi ningekuwa msichana Broo Magu, ningetoa kidogo tu ningeambiwa nafasi zipo.Maana nimekomaaa nikasema aliyekwambia utafte watu ndo ameniambia nije unifanyie interview, eti mshikaji mmoja kakomaa. Nikamwelekeza msichana, CV imepokelewa.

Broo Magu futa mitandao ya ajira, ajira zibakie mikononi mwa serikali na wakala wake. Hili litaingizia nchi pesa nyingi sana.

Naomba kuwakilisha mzee Broo Magu.

Waziri wako simjui jina ila naomba asome waraka.
 
Nahic ombi lako Mh Rais amelisoma.
Maana sasa yupo home town (chato) amepunzika likizo ya wiki moja
 
Nahic ombi lako Mh Rais amelisoma.
Maana sasa yupo home town (chato) amepunzika likizo ya wiki moja
Hivi rikizo yake nan anaaprove sisi tlio mchagua ndo tulitakiwa tuaaprove, nimesema asome na anijibu mi najua yupo, umu id yke imedilika siku hizi
 
hivi rais anaweza kuwa yumo humu jf au
hawezi kukosa ingawa siu hizi speed ya kuingia imepungua ila anaingiaga maana wakati wa kampeni ndo nilijua kuwa yumo humu labda kama katoka baada ya kuwa raisi.
 
umekosea si TEMESA NI TaESA kama sijakosea, TEMESA ni wakala wa ufundi na umeme(Tanzania Electrical, Mechamical and Electronics Services Agency)
asante kwa kunikosoa, ila ujumbe umeupata na unasemaje?
 
the best way kuongeza uwajibikaji na kupanua fursa za ajira ni kupunguza umri wa kustaafu tu....umri ukishuka mpaka at least 45yrs watu watakuwa serious kutumia vizuri hela zao za mishahara na sio kuhonga na kukopa magari makali na badala yake watazitumia kuwekeza na kujijenga kiuchumi kujiandaa kuyakabili maisha pindi watapostaafu...heshima ya kazi pia itakuwepo coz mtu atakuwa na adabu akfikiria kuupoteza hata mshahara wa miezi miwili ya kazi kwa kusimamishwa
 
ila jaman tuwe wakweli tanzania hii inaajira nying serikalin ila shindwa kuelewa kwanin wanabana.
 
sectir ya ardhi ina matatzo meng yanahitaji vijana lakin vijana hao hawaijiliwa .mfano vijana wanaotoka chuo kikuu ardhi wapekwe huko na wasamiwe vizuri.offc zimejaa wazee wered umepungua software matumiz yake hawajui lakin et ajira ni tatzo.
 
the best way kuongeza uwajibikaji na kupanua fursa za ajira ni kupunguza umri wa kustaafu tu....umri ukishuka mpaka at least 45yrs watu watakuwa serious kutumia vizuri hela zao za mishahara na sio kuhonga na kukopa magari makali na badala yake watazitumia kuwekeza na kujijenga kiuchumi kujiandaa kuyakabili maisha pindi watapostaafu...heshima ya kazi pia itakuwepo coz mtu atakuwa na adabu akfikiria kuupoteza hata mshahara wa miezi miwili ya kazi kwa kusimamishwa
Hii ni safi sana japo wengi wataichukia. Kwa maofisa wa kawaida umri uwe 45 na vyeo vya wakurugenzi na watendaji wakuu wa taasisi umri uwe hadi miaka 50 hivi. Hapo kila mtu atajituma kujiajiri na pia fursa za ajira zitakuwa nyingi sana serikalini.
 
Umesema vyema mkuu hope magu amesikia Na atalifanyia kazi lakini hii nchi kwa kweli inahitaji reforms ya hali ya juuu.
 
Hii ni safi sana japo wengi wataichukia. Kwa maofisa wa kawaida umri uwe 45 na vyeo vya wakurugenzi na watendaji wakuu wa taasisi umri uwe hadi miaka 50 hivi. Hapo kila mtu atajituma kujiajiri na pia fursa za ajira zitakuwa nyingi sana serikalini.
Mi nadhani maofisa wa kawaida iwe 50 kwa kuwa wanamishahara midogo na wakurugenzi na watendaji wakuu iwe 45 kwakua ndo wanakula hela ndefu.
 
wazo lina lengo zuri,sema lina kauchachu...ule mfumo wakufanya interview- mitahan DUCE na Oral-interview Uwanja wataifa ndio unataka utumike kwa watu binafsi?Hivi huu mfumo utapata mfanyakazi bora kweli ndugu yangu?Sekta binafsi ziko serious kuona more impact siku zote lazima wahakikishe wana the right canditate sio vyet na kufaulu mitihani
 
Back
Top Bottom