Waraka wa wazi kwa Prof. Ibrahim Lipumba

Waraka wa wazi kwa Prof. Ibrahim Lipumba

keynessian

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
591
Reaction score
422
Habari za wasaa huu mchumi mwenzangu Lipumba,

Tunaheshimu uamuzi wako wa kujiuzulu uliouchukua hivi karibuni, ni simanzi kubwa kwa wanaharakati wa mabadiliko nchini.

Kitendo hichi mpaka sasa kimezua maswali maswali mengi kuliko majibu,kimefanya juhudi zako zote za kupigania mabadiliko kuwa sawa sawa na hamna kitu, lakini pia umejivunjia heshima yako kubwa ulijiwekea kwa muda mrefu wananchi walitarajia mtu mwenye busara kama wewe ambayo umejitokeza mara nyingi kuwania nafasi ya urais kwamba utakuwa ni mtu mwenye busara na hekima kubwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi kwa kutambua athari ya maamuzi yako kwa sasa na baadaye.

Ni aibu sana kwa mwanazuoni mkubwa kama wewe kutoa excuse kwa kusema dhamira yangu inanisuta. Vipi kama ungekuwa kiongozi mkuu wa nchi ni maamuzi mangapi ya hovyo ungeyefanya na kusema dhamira yako imekusuta?

Hii wanazuoni wanaiita intellectual negligence, umeeonesha udhaifu mkubwa sana kwenye maamuzi,umedhalilisha taaluma na ninasema bila kumungunya hauna sifa ya kuwa kiongozi.

Aidha nipende kutoa shukrani kwa dhati kwa watanzania waliokukataa kwenye sanduku la kura miaka yote uliyogombea, lakini lingine ambalo ni likubwa nawashukuru sana viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif pamoja na wanachama wote wa CUF kwa kukupuuza wewe pamoja na kitendo chako cha kujiuzulu.

Ushauri wangu kwako: Kuendelea kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kuponda UKAWA ni kuendelea kujivunjia kale kaheshima kadogo kalichobakia,ingekuwa busara zaidi kama ungekaa pembeni na kuwa mtazamaji.

Ni hayo tu.

Keynessian!
 
Huyo Laprofeseri hatambuliki tena katika medani za kisiasa.Wasifu wake umeingia dosari.
 
Linanaonekana linakula bata Rwanda na watoto wa kigogo nchini ndio maana alina mke ----- sana
 
Hicho kitendo chake cha kujiuzulu "hakijazua maswali mengi" yeye aende zake tu...uzuri vitani kuna askali huwa "wanatekwa" ndo kama yeye sasa.
 
kwani yeye ni nani,maamuzi yake magum,atayajutia,ni kusonga mbele,ajitambue yy alikua kikwazo
 
Huyo Lipumba wala dhamira haijamsuta. Maamuzi yake ya kujiuzulu yametokana na rushwa ya CCM!
 
Lipumba nimemdharau anatupa makombora na tuhuma akiwa huko nyumbani kwake rwanda tena abaki huko kwani hatumtaki tena huyo mnafiki Lipumba tena
 
Wala sio dhamira kumsuta.ni kaziraa baada ya kukosa nafasi ya kugombea urais hana lolote
 
Anakula pension yake huko aliko aliyolipwa na ccm. Kuitumikia ccm ukiwa chini ya kapeti la upinzani si kazi ndogo ati! Alikuwa anatuchora tu na kutuhadaa na sauti yake ile. Na hata kuwasababishia wenzake wapigwe na polisi na kufunguliwa mashtaka ilikuwa sehemu ya mission yake kwa ccm. Hana maana hata kidogo. Tutayajua mengi juu yake muda ukifika.
 
nina uhakika wewe ni chekechea kwa Lipumba na hata kujiita mchumi mwenzako ni upuuzi tu maana huna hiz sifa. siku hizi hata walinzi mnajiita wachumi. upuuzi wa aina yake huu. na tangu lini umekuwa ukimsapo Prof? baada ya kujiunga na mabwana zenu aknia mbowe? ni mara ngapi mmekuwa mkimdhihaki Seif? leo hii kwa kuwa anaendana na interest zenu ndo anaonekana anafaa? eti unapenda kumpta ushauri, wewe nani mpaka umpe ushari? eti ni aibu? hiyo aibu umeiona wewe tu? na hao nyumbu wenzako? tuondolee hiki kinyesi chako hapa.

Habari za wasaa huu mchumi mwenzangu Lipumba,

Tunaheshimu uamuzi wako wa kujiuzulu uliouchukua hivi karibuni, ni simanzi kubwa kwa wanaharakati wa mabadiliko nchini.

Kitendo hichi mpaka sasa kimezua maswali maswali mengi kuliko majibu,kimefanya juhudi zako zote za kupigania mabadiliko kuwa sawa sawa na hamna kitu, lakini pia umejivunjia heshima yako kubwa ulijiwekea kwa muda mrefu wananchi walitarajia mtu mwenye busara kama wewe ambayo umejitokeza mara nyingi kuwania nafasi ya urais kwamba utakuwa ni mtu mwenye busara na hekima kubwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi kwa kutambua athari ya maamuzi yako kwa sasa na baadaye.

Ni aibu sana kwa mwanazuoni mkubwa kama wewe kutoa excuse kwa kusema dhamira yangu inanisuta. Vipi kama ungekuwa kiongozi mkuu wa nchi ni maamuzi mangapi ya hovyo ungeyefanya na kusema dhamira yako imekusuta?

Hii wanazuoni wanaiita intellectual negligence, umeeonesha udhaifu mkubwa sana kwenye maamuzi,umedhalilisha taaluma na ninasema bila kumungunya hauna sifa ya kuwa kiongozi.

Aidha nipende kutoa shukrani kwa dhati kwa watanzania waliokukataa kwenye sanduku la kura miaka yote uliyogombea, lakini lingine ambalo ni likubwa nawashukuru sana viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif pamoja na wanachama wote wa CUF kwa kukupuuza wewe pamoja na kitendo chako cha kujiuzulu.

Ushauri wangu kwako: Kuendelea kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kuponda UKAWA ni kuendelea kujivunjia kale kaheshima kadogo kalichobakia,ingekuwa busara zaidi kama ungekaa pembeni na kuwa mtazamaji.

Ni hayo tu.

Keynessian!
 
mtaongea mengi sana mpaka mpasuke vichwa! Watanzania tulisha amua suku nyingi kwamba mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko hata kama ukawa atagombea mchina sisi tunampa kura kuliko kuendelea kunyanyaswa na ccm, angalia hii migodi afu uihurumie nchi:buzwagi gold,shanta gold,north mara gold,buly gold,nzega resolut gold,ggm,nchi ya arab emirates kule serenget na loliondo maliasili inapigwa mbaya!. Bora hao ni watanzania yaani hata ukileta mzungu ukawa tunampa.tumechokatumechoka !!we endelea kula hivyo vya mwisho kimsingi tafuta namna ya kujiajiri mapema maana njia zako zote za kuliibia taifa tunakwenda kuzikata!!!

mbona unampa makavu ukawa mwenzio
 
kheri hivyo alivyoondoka kibaraka huyu maana alitaka apeperushe bendera ya ukawa na halafu aje amwage vimbwanga one week be4 election na awaache ukawa wakiwa uchi bila ya mgombea
 
Nashauri CUF wamvue uanachama haraka kwani amekuwa msaliti.Hafai kubaki upinzani.
 
​Nimeona picha zake zinasambaa akiwa na kijana anayeaminika ni wa system wakila bata rwanda
 
Back
Top Bottom