Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,018
- 20,489
Historia ya siasa duniani haitengani na historia ya dini. Vitu hivi vimekuwa sambamba na vyenye mafaa kwa jamii yoyote ile duniani, lakini vikileta matatizo makubwa sana katika baadhi ya nchi duniani, matharani ubaguzi wa kiimani umeleta machafuko na uharibifu mkubwa mali pamoja na mauti dhidi ya binadamu. Vitu hivi imekuwa ni vigumu sana kutenganisha katika dunia ya leo huku machipuko ya kiimani yakija kwa kasi ya ajabu.
Kwa upande wa Tanzania mfumo wa siasa umekuwa ni wa kuakisi kutoka mataifa ya Magharibi, na uakisi wake umekuwa ni kinyume. Tukiangalia historia ya binadamu tunaona yakuwa kabla binadamu hajajishughulisha na masuala ya siasa na utawala alikuwa anajishughulisha na maswala ya dini, binadamu akawa mcha-Mungu.
Ulipofika wakati wa uteuzi wa kiongozi wa jamii mtu aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa ni yule aliyeonekana ni mcha-Mungu. Hata katika jamii zetu za kiafrika zilizotuletea kiongozi wa utawala, pia alikuwa kiongozi wa dini.
Ni huyu aliyeongoza shughuli zote za utawala na za dini katika jamii. Itatumika biblia kutoa mifano hai kuthibitisha uhusiano wa dini na siasa. Hakuna ubishi dunia inakubali yakuwa Yesu Kristo ndiye mwanzilishi wa dini ya kikristo. Hii ni kusema kuwa Yesu Kristo alikuwa kiongozi wa dini. Kwaupande wa kabila Yesu alikuwa Muebrania.
Alipozaliwa nchini Uyahudi alikuta tayari watu wa kabila lake wanadini yao ya kiyahudi. Viongozi wa dini ya kiyahudi walikuwa pia watawala waliotawala kwa kutumia sheria za kiyahudi zilizomo katika kitabu chao cha sheria kiitwacho TORATI sheria hizo za dini zikawa pia sheria za utawala.
Warumi walipoanzisha utawala wao, Wayahudi waliwaruhusu Warumi kufuata sheria zao za dini ambazo pia zilikuwa sheria za utawala wao wa jadi. Kuhani Mkuu ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa dini, alikuwa mwenyekiti wa Baraza kuu la utawala lililoitwa Sanhedrin.
Ni baraza hilo ndilo lililotoa hukumu kuwa Yesu auawe (Math 26:65-69). Hata hivyo adhabu yoyote ya kifo iliyotolewa na baraza kuu la wayahudi ilibidi ithibitishwe kwanza na mtawala wa Kirumi kabla haijatekelezwa (Yohana 18:31).
Kwa upande wa Yesu Kristo alipoanza kufundisha dini yake mpya alikosoa sheria za kiyahudi ambazo aliziona hazikuwasaidia binadamu kuishi kwa upendo na amani. Aliwataka wafuasi wa dini yake mpya wasiwe na tabia ya kulipa kisasi. Kwamfano sheria za kiyahudi zinasisitiza kauli ya jicho kwa jicho na jino kwa jino.
Katika (Math 5:38-41) tunasoma yakuwa Yesu hakutaka sheria hizo, alisema, “Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino, lakini mimi nawaambia msishindane na mwovu lakini mtu akupigae shavu la kuume mgeuzie na la pili na mtu atakaye kushitaki nakuitwaa kanzu yako mwachie na joho.
Uongozi safi wa kidini wa Yesu Kristu uliwavutia wayahudi wa kawaida hata wakaona anafaa kuwa kiongozi wa utawala, wakataka kumfanya awemfalme. Lakini Yesu hakuwa tayari kujiingiza mno katika masuala ya siasa na utawala (Yohana 6:15) alizoea kusema ufalme wake sio wa ulimwengu huu (Yohana 18:36) Katika mafundisho yake, Yesu hakuwahi kuwaambia wafuasi wake wasichanganye dini na siasa. Hata hivyo aliwataka wawe waangalifu katika kuyashughulikia masuala hayo mawili. Alisema, “Ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu”. (Luka 20:25).
Hakuwahi kuwataka wafuasi wake washughulike na mambo ya mungu (dini) tu wasijishughulishe na siasa. Katika hali hii niwazi kuwa kiongozi wa dini hatakiwi kuhubiri siasa katika jengo la ibada akaacha mambo ya mungu. Vilevile anapokuwa nje ya jengo la ibada hana mwiko wakutokuzungumzia masuala ya siasa na utawala.
Baada ya kufa Yesu, wafuasi wake waliendelea kujihusisha na masuala ya dini na siasa, mambo ya utawala yakiendelea kuhusishwa na dini. “Iliaminika kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu (Warumi 13:1). Katika hali hiyo kiongozi wa Katoliki duniani Papa wa Roma alipewa mamlaka makubwa ya utawala, eneo lake la Vatican likapewa hadhi ya utawala wa nchi.
Eneo hilo likapewa mamlaka kamili yakupokea mabalozi wakigeni. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na imani ileile iliyojengeka siku nyingi kuwa kiongozi wa dini ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa utawala pia maana kwanjia hiyo atakuwa nanafasi nzuri ya kupambana na maovu.
Lakini wakati Papa wa Roma anashughulikia zaidi masuala ya dini kuliko ya siasa na utawala, kuna viongozi wengine wa dini wamewahi kupewa madaraka kamili ya kushika utawala wa nchi. Mfano Askofu Mkuu Makarios wa kisiwa cha Cyprus ambaye aliwahi kutembelea Tanzania.
Wakati huohuo kuna nchi duniani ziliamua siku nyingi kuwa nchi za dini mfano Uingereza ni nchi ya kikristo ambapo mishahara ya maaskofu hulipwa na serikali. Pia nchi za Saud Arabia, Moroco, Libya nk ni nchi za kiislamu. Si hivyo tu pia kuna nchi ambazo vyama vya siasa vya kidini vinaruhusiwa mfano Ujerumani Christian Democratic Union (CDU.
Uongozi hutoka kwa watu, Watu ndio wanaweza kukufanya kuwa kiongozi, Ukiona watu wamekuja kukuomba uwe kiongozi wao tena watu hao "wenye tashwishwi na haiba za nera (mvi)" tambua kuwa mamlaka hiyo inatoka kwa Mungu. Pindi uachapo uongozi na kujitwika utawala, Mungu hujitenga nawe na shetani huambatana nawe, Utawala huenenda na damu, uongozi huenenda tabasamu la moyo na vinywani mwa umma.
Ni hayo rais wangu, sikia sauti ya Mungu kupitia makutano yaliyofika mbele yako kukupa uongozi! Tunamtaka Ben Saanane akiwa hai.
Na Yericko Nyerere

inaweza kuwa kichekesho