Waraka mzito kwa Katibu Mkuu CCM Taifa, Dr. Ally Bashiru

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
KATIBU MKUU,
WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
S.L.P 50
DODOMA.

YAH: MALAMIKO DHIDI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Bashiru Ally, sisi ni baadhi wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, tunachukua fursa hii kupitia barua yetu kuleta malalamiko yetu kwako kuhusu yaliyojiri katika semina elekezi (retreat) iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo Januari 19-21 2020 wilayani Karatu.

Mheshimiwa Katibu Mkuu, Kikao kilifanyika kwa siku 3 ambapo siku ya kwanza wajumbe takriban 61 walitembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na kila Mjumbe alilipwa Posho ya kikao @300,000, Malazi, Chakula na Usafiri wa kwenda na kurudi kwa kutumia magari ya serikali na ya binafsi.
Pia, wajumbe wote walilipwa posho ya shilingi 80,000 kila moja na ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha.

Kwa mujibu wa mwaliko wa Mkuu wa Mkoa, lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutengeneza mahusiano na waliotoa mafunzo Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Musa Matoroka, Afisa Takukuru Mkoa wa Arusha, na Afisa Maadili Mkoa.

MALAMIKO:
Mheshimiwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa kama tulivyoeleza hapo awali, lengo la waraka huu ni kuleta malalamiko yetu kwako kama Mtendaji Mkuu wa chama dhidi vitendo vilivyojiri vya ukiukwaji wa Katiba,Kanuni,na Taratibu vilivyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Sisi kama viongozi na wanachama wa CCM tunaamini kuwa tunaowajibu wa kulinda Katiba,Kanuni,Taratibu na miongozo inayosimamia chama chetu ili kuwa mfano mbele ya jamii na pia vyama vingine vya siasa.

1.Mheshimiwa Katibu kilichotushangaza semina hiyo hiyo iligeuka kuwa kikao cha Mkuu wa Mkoa ambapo alitumia zaidi ya masaa matatu kueleza kazi alizofanya badala ya malengo ya awali tuliyoelezwa ya kujenga mahusiano.

2.Kikao hicho pia kilitoa jukwaa kwa Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige kueleza kazi zake kwa masaa matatu lakini Mbunge mwingine Amina Mollel alinyimwa fursa hiyo hali iliyoleta vurugu kwa baadhi ya wajumbe na mbunge Amina kuangua kilio mbele wajumbe.Mh Catherine na Mh Rc Mrisho Gambo wamekuwa wakigawa cha.

kwa muda mrefu kwa maslahi yao binafsi na kuumiza makada mbalimbali waaminifu na watiifu kwa ccm mkoani Arusha na mbaya zaidi wamemwingiza mkiti mpya wa mkoa ndugu Zelote na katibu wa mkoa Ndugu Musa Matoroka katika harakati za kukigawa chama cha mapinduzi katika mkoa wa Arusha.

Hata hivyo amewatengeneza baadhi ya viongozi wa dini na wazee na wafanyabiashara hasa wahindi wakiongozwa na Shekh mkuu wa mkoa wa Arusha ili kumtengenezea sifa kumwomba kuwa mgombea Moja ya majimbo ya mkoa Arusha.Kama viongozi tunahisi kupewa rushwa.Na mmoja wa wafadhili wake ni wahindi na Mhifadhi NCAA Nd Manongi mkuu wa hifadhi ya Ngorongoro.

Mheshimiwa Katibu Mkuu tunaamini hatua ya Mbunge Amina Mollel ambaye kimsingi ana Hadhi sawa na Magige hakijafanywa kwa bahati mbaya.Ni maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ili kutoa nafasi ya upendeleo kwa Magige ambaye ni mshirika wake kisiasa.Pia kulikuwa na nia mbaya ya kumdhalilisha Mbunge Mollel mbele ya wajumbe ili kumvunja nguvu kisiasa, tunaamini kuwa Katiba ya chama chetu hairuhusu ubaguzi kwa Mbunge huyo ni mwakilishi wa kundi nyeti la walemavu.

3. NMheshimiwa Katibu Mkuu pia tumesikitishwa na tunalalamikia vitendo walivyofanyiwa wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Arusha Neema Mollel na Jasmin Bachu ambao awali walifanyiwa maandalizi ya vyumba (bookings) katika hoteli mbili tofauti lakini kila walipofika ilionekana majina yao yako kwenye kitabu cha wageni vyumba vilikuwa na watu.

Baadaye wajumbe hao walipelekwa hoteli iliyoko vichochoroni na walipopatiwa vyumba baadaye ilibainika kuwa kulikuwa mpango ovu dhidi yao (kubakwa) unaodaiwa kusukwa na kuratibiwa na RC Gambo kutokana hatua ya wajumbe hao kutofautiana yeye Gambo mara kwa mara katika vikao vya kamati ya siasa ya Mkoa.

Wajumbe hao baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wasmaria wema waliondoka katika hoteli hiyo na kwenda kutafuta malazi sehemu nyingine.

Mheshimiwa Katibu Mkuu kwa madai hayo RC Gambo ni kiongozi anayekosa uvumilivu wa kisiasa kwa viongozi wenzake ambao wanatofautiana kimawazo na ni kiongozi ambaye anakosa maadili ya kiuongozi.

4.Mheshimiwa Katibu Mkuu siku iliyofuata RC Gambo alitoa lugha matusi kuwa kuna baadhi ya wajumbe waliopatiwa malazi ni wapumbavu, wahuni na Malaya akiwalenga wajumbe hao wawili waliobadilisha hoteli baada ya kupata taarifa hizo kuwa wangefanyiwa vitendo vibaya na wajumbe hao walipotaka kuzungumza kujitetea Mwenyekiti wa kikao Zelothe Steven aliwapuuza kwa kuwanyima nafasi.

Wajumbe hao pia walikataa kupoea posho ya shilingi 300,000 na kurudisha fedha hizo lakini RC aliwakatalia.Mheshimiwa Katibu Mkuu tunashawishika kuamini kuwa Mkuu wa Mkoa kwa nafasi yake na kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma haruhusiwi kutoa lugha ya matusi mbele ya hadhara.

5.Mheshimiwa Katibu jambo la kusikitisha katika hichoMadereva walinyimwa chakula na posho ya Malazi jambo ambalo ni kinyume na utu na haki za binadamu na chama chetu na kibaya zaidi Katibu Mwenezi wa chama Mkoa wa Arusha Gerald Munisi ambaye ni mshirika wa RC Gambo alitoa lugha ya chafu dhidi yao kuwa hawastahili kula na chakula ni kwa ajili ya viongozi tu.

7.Msheshimiwa Katibu Mkuu sisi tunaamini kuwa RC Gambo aliandaa semina hiyo kwa malengo na manufaa yake binafsi kwanza kumwaminisha Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Steven kuwa katika kambi yake ya kisiasa na pia kuwashawishi wajumbe waliokuwa wakijiandaa kwenda kuonana Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.John Pombe Magufuli (Januari 23,2020) ili wasimseme vibaya kutokana na utendaji kazi wake mbaya hapa Arusha.

HITIMISHO:
Mheshimiwa Katibu Mkuu sisi wajumbe wa Halmashauri Kuu, tumesikitishwa na kufadhaishwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya chama chetu vinavyofanywa mara kwa mara na RC Gambo ambayo kimsingi imeleta mpasuko na mgawanyiko ndani ya CCM Mkoa wa Arusha jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa chama chetu kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020.

Mheshimiwa Katibu Mkuu sisi viongozi na wanachama tumekuwa tunajiuliza malengo ya RC wetu ni nini hasa? Tangu lini semina ya elekezi ya chama tena Halmashauri kuu ya mkoa kugharamikiwa na Rc –
Kwanini retreat igeuzwe kuwa sehemu ya kuelezea utekelezaji wa ilani wakati haikuwa mahali pake?
Kwanini Mbunge mmoja apewe kueleza kazi zake mkoani na mwingine kunyimwa fursa hiyo?

Kama wajumbe wa Halmashauri Kuu wanasafirishwa na kupelekwa tour na Mkuu wa Mkoa na kulipwa posho yenye aina zote za harufu ushawishi wa kuwanunua ama kuwanyamazisha na kumsifia?
Dhana ya chama kusimamia serikali na wateule ili kutimiza wajibu wao kwa chama inatekelezwaje?
Kwanini retreat haikuandaliwa na chama Mkoa badala ya RC na fedha tulizolipwa na RC zimetokana na nani?

Waliotoa usafiri,malazi na chakula bure ni akina nani wana malengo gani na chama chetu?
Je, hii si rushwa kwa wajumbe mbeleni ukizingatia wengine na watia kwenye uchaguzi huu?
Tunaomba ofisi ya Katibu Mkuu kufanya uchunguzi juu ya hali ya ccm mkoani Arusha hasa kipindi hiki tunakoelekea uchaguzi mkuu 2020.

ASANTE
TUNAOMBA KUWASILISHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chema chajiuza, kibaya chajitembeza. Ila niwaume tu sikio makada mliojawa na uchungu na kuguswa na suala hilo, siku nyingine ni vyema taarifa kama hizi zikawakilishwa kwa faragha ili zipate kushughulikiwa kimya kimya ndani vikao husika vya chama bila ya umma kutambua. Ukitaja hadharani mambo ya ndani ya familia yako ni kama unajidhalilisha mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama kinachoongoza kwa kutoa na kupokea rushwa Africa ni CCM

Rushwa ipo kote. Sema hyo barua Mbona Kama imeandikwa kitoto sana. Afu kama Ni kwa katibu hapa imefikaje. Hakuna mwanachama anayependa kukiabisha chama chake. Ndo mna CHadema Hakuwa na Shida na uenyeketi wa kudumu.
 
Rushwa ipo kote. Sema hyo barua Mbona Kama imeandikwa kitoto sana. Afu kama Ni kwa katibu hapa imefikaje. Hakuna mwanachama anayependa kukiabisha chama chake. Ndo mna CHadema Hakuwa na Shida na uenyeketi wa kudumu.
Wewe bwege nini hapa cdm inaingiaje?
Tatueni matatizo yenu wenyewe

In God we Trust
 
Back
Top Bottom